Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd Bw. Chengal Reddy. Dkt Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ludigija.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani akikagua chupa za maji katika Kiwanda cha A One product and Bottles Vingunguti, Dar es Salaam kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani akitoa
maelekezo kwa Bw. Chengal Reddy
Mtendaji Mkuu wa Kiwanda
cha A One product and Bottles cha Vingunguti, Dar
es Salaam, hukakisha chupa za rangi zinakusanywa, kurejeshwa kiwandani na
kurejelezwa na kutengeneza bidhaa nyingine.
Serikali imesema kamwe haitakuwa kikwazo kwa
wawekezaji wanaolenga kuwekeza katika sekta ya viwanda bali maendeleo ya
viwanda ni lazima yaende sambamba na hifadhi ya Mazingira.
Rai hii imetolewa leo Februari 24, 2022 na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani
Jafo katika ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira
katika Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd katika Mkoa wa
Dar es Salaam.
Dkt. Jafo amesema Serikali inahimiza wawekezaji
nchini lakini ni vema wawekezaji hao wazingatie Sheria ya Usimamizi wa Mazingira
kwa ukamilifu wake. Katika ziara ya kukagua kiwanda hicho kinachozalisha
vinywaji baridi (soda, maji na juisi). Waziri Jafo amepongeza utii wa Kiwanda
hicho kwa kutekeleza kwa wakati maagizo ya Serikali ya kutotumia karatasi za
plastiki kwenye vifuniko vya chupa za maji.
“Kiwanda hiki kimenifurahisha sana, wametii kwa
vitendo maagizo ya Serikali ya kutotumia karatasi za plastiki kwenye vifuniko
vya chupa za maji yanavyozalishwa na Kiwanda hiki. Kiwanda hiki pia kimeanzisha
kiwanda cha kurejeleza chupa za plastiki,
hata zile za rangi ambazo ukusanyaji wake umekuwa na changamoto, natoa rai kwao
kuhakikisha chupa zao hazisambai katika mazingira bali wanazirejesha kiwandani
na kutengeneza bidhaa nyingine”
Amesema, viwanda vina mchango mkubwa sana
katika kukuza uchumi wa nchi sambamba na kuchangia ajira za moja kwa moja hivyo
Serikali itahakikisha matakwa ya Sheria yanazingatiwa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha A
One product and Bottles Ltd Bw. Chengal Reddy amesema wamefanya
jiitihada za dhati katika kuhakikisha chupa za rangi zinazozalishwa kiwandani
hapo zinarudi katika mzunguko kwa kutengeneza bidhaa nyingine.
“Tuna kiwanda kingine Mbagala ambapo chupa hizi
za rangi zinachakatwa na kutengeneza bidhaa nyingine za plastiki kama vile Busati
na shedi za Magari” Alisisitiza Bw. Reddy.
Mapema mwezi Oktoba 2021 Serikali ilipiga marufuku matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal) na vinywaji baridi kwani ni hatari kwa mazingira na viumbe hai kwa kuwa hazirejelezeki na kuathiri ikolojia ya raslimali maji na ardhi.
Post a Comment