MANARA ALA SHAVU BODABODA MKOMBOZI KWA WATANZANIA.

 


Balozi wa Kampuni ya Sunbeam wanauza bidhaa ya Pikipiki aina ya hunter Haji Manara akijaribu pikipiki"Chombo ya kijanja" Jiji dar es salaam.




    Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WATU Wenye ushawihi katika jamii washauriwa kuheshimu na kujenga nidhamu ya Hali ya pindi wanapoteuliwa kuwa Mabalozi katika Makampuni.


Akizungumza hayo Balozi wa Kampuni ya Sunbeam yenye chapa ya pikipiki ya Hero Haji Manara amesema mara nyingi Kampuni zimekuwa zikitoa fursa za watu wenye ushawihi kwenye jamii kuzitangaza Kampuni hizo hivyo waonyeshe juhudi na kuwaaminisha kuwa wamefanya uchaguzi sahihi katika uteuzi huo.


Haji Manara mapema Leo, ameteuliwa kuwa Balozi wa Kampuni hiyo na kuibeba rasmi Kampeni ya "Piga gia Barabara ishangae".


Pia ahaidia kufanya kazi Kwa ushirikiano mkubwa na Kampuni hiyo Huku akisisitiza swala la kutoa Elimu Kwa madereva wa pikipiki kutumia "kofia" Kwa usalama wao na abiria Ili kupunguza Kasi ya ajali za Barabara.


Aidha,Meneja Masoko wa Kampuni hiyo ambayo mpaka Sasa imeshasambaza takribani pikipiki  milioni 1 duniani,Nadah Dhiyebi amesema Kampuni ya Hero Motorcorp inaongoza Kwa kutengeneza na kuzalisha pikipiki zinazoongoza Kwa ubora duniani.


"Pikipiki zinapatikana nchi nzima Kwa Mawakala wajiosajiliwa ambapo mpaka Sasa wapo Mawakala 27 wapo Kwa ajili ya kukuhudumia."


Hata hivyo Dhiyebi ameeleza kuwa bidhaa hizo zimekuja kuwakomboa watanzania Kwa kuingiza nchini pikipiki za Hunter ambazo ni hunter 100 .


....done...

0/Post a Comment/Comments