SERIKALI YAOMBWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA KILIMO ILI KUKUZA SEKTA HIYO.

Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya JATU PLC Mohamed Simbano  wakati  akizungumza na waandishi wa habari walipoingia makubaliano  ya  kumteua   Msanii  Mrisho  Mpoto kuwa  balozi kwa miaka mitatu

Mrisho Mpoto ambaye aliyeteuliwa na waziri wa Maji Jumaa kuwa balozi wa Sekta ya Maji akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam

............................

NA MUSSA KHALID

Serikali imeombwa kutambua mchango wa wadau binafsi katika kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini ambayo imekuwa ikiongoza katika kutoa ajira kutokana na rasilimali zinazozalishwa kutumika kwa ajili ya shughuli za biashara pamoja na kilimo.

Hayo yameelezwa leo  Jijini  Dar es Salaam   na  Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya JATU PLC Mohamed Simbano  wakati  wakiingia  makubaliano  ya  kumteua   Msanii  Mrisho  Mpoto  kwa   kuwa  balozi kwa miaka mitatu ili kutangaza  sekta ya maji ambayo inaendana sambamba na kilimo cha kisasa.

Mohammed  Simbano  amesema  Jatu Plc katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kutekeleza  na kuendeleza miradi ya maendeleo ya  serekali, Kampuni  hiyo  imekuwa ikitoa  kipaimbele  katika na sekta  ya  maji kwa kuwa ndiyo  nguzo  muhimu katika  kilimo cha kisasa.

Aidha  Simbano  amesema  kupitia utaratibu uliopo katika taasisi hiyo, wameweka njia nzuri za kumuwezesha kila mkulima kumiliki ardhi na kuwa na matumizi bora ya ardhi huku  wakiiomba  Serikali  kuishika  mkono Jatu Plc kwa kuchochochea  maendeleo  ya  Taifa  kwa  kulipa  kodi  mbali mbali.

Kwa upande wake Mrisho Mpoto ambaye aliyeteuliwa na waziri wa Maji Jumaa kuwa balozi wa Sekta ya Maji amewaomba watanzania kuendelea kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga  mkono  Rais  Samia  Suluhu  Hassan katika  kuwaletea maendeleo  wananchi.

‘Lengo langu ni kuhakikisha naendelea kuonyesha ushirikiano kwa serikali katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ambapo nitaendelea kuzungumza kuhusu yanayotekelezwa na serikali hivyo natoa fursa kwa wadau mbalimbali kuunga mkono suala hilo’amesema Mpoto

Mrisho Mpoto ameteuliwa kwa mara nyingine kuwa Balozi wa JATU PLC kwa kipindi kingine cha miaka mitatu  ili kuendelea kutangaza miradi mbambali inayofanywa chini ya  Rais  Samia  Suluhu  Hassan  hasa  miradi  ya  maji  na  kilimo  ili  kukuza  uchumi wa  Taifa  na  mwananchi  mmoja  mmoja.

0/Post a Comment/Comments