TAASISI ZA KIDINI ZATAKIWA KUUNGA MKONO MAPAMBANO YA KORONA KUPITIA TUNGO


...........................................

NA SALYM BITCHUKA

Taasisi  za  kidini  nchini zimetakiwa  kujitokeza  na  kumuunga  mkono  Rais  wa Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Samia  Suluhu  Hassan  katika   Mapambano  ya  Uviko - 19 .

Hayo  yamebainishwa  leo  Jijini  Dar  es Salaam   wakati  wa  uzinduzi  wa  Mashindano  ya Qaswida  zenye  tungo zinazohusu  Corona ikiwa  ni  pamoja  na  kuchanja   pamoja  na  kuchukua  tahadhari  zake  nyingine.

Akizungumza  katika  Uzinduzi  huo  Mganga  mkuu  wa Mkoa  wa  Dar es Salaam Dkt. Rashid  Mfaume   amesema  Kupitia  tungo  hizo za Qaswida  zitasaidia  kufikisha  ujumbe  kwa  jamii  na  kuelimisha  jamii  ya Kitanzania  katika  kuchukua  tahadhari  ya  uviko -19  kwa  kuchanja.

Kwa upande  wake  Mwenyekiti  wa  Jumuiya  ya  vijana  Bakwata  taifa Alhaji  Muharami  Hamisi  pembe  amesema  mashindano  hayo ni  maalum mkwa  vijana  wenye  vipaji  vya  kuimba  ili  waonyeshe  vipaji  huku  wakihamasisha  jamii  kujilinda  na  kuchukua  tahadhari  dhidi  ugonjwa  wa Corona  unaosababishwa  na  vijidudu vya  Covid – 19.

Nae  Mwakilishi  kutoka  shirika  la  MDH  ambaye  ni  msimamizi  wa  Miradi  ya  MDH  Mkoa wa  Dar  es Salaam   Dkt. Alli  Kaduma  amesema wameamua  kuwasaidia  Baraza  la  Vijana katika  mashindano  hayo  kutoka na  lengo  lao  la  kuhamasisha  jamii kuchukua  tahadhari  kupitia  tungo  za Qaswida  kwa  kuwa  takwimu  zinaonyesha  walio wengi  ambao  wamelazwa  kutokana  na  ugonjwa  wa  Corona  ni  wale  ambao  bado  hawajachanja.

Mashindano  haya  ya  Qaswida  zenye  tungo za  Uviko – 19  yamezinduliwa  leo  Februari  09 ,2022  na  fainali  zikitarajiwa  kufanyika  mwishoni mwa mwezi  wa  March  mwaka  huu ambapo  leo  washiriki  mbali mbali  wamejitokeza  huku  wakighani  tungo  zilizosheheni  maneno  ya  kuhamasisha  watu  kuendelea  kuchukua  tahadhari  mbali mbali  dhidi  ya  Uviko – 19.

0/Post a Comment/Comments