TBS YAWATAHADHARISHA WAFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA CHAKULA.


Afisa Uthibiti ubora TBS, Baraka Mbajije wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS, Ubungo Jijini Dar es Salaam.

.........................................

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewatahadharisha wafanyabiashara bidhaa za chakula zilizofungashwa yakiwemo mafuta ya kula kuweka ama kuanika kwenye jua kwani kunaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya kwa binadamu.

Ameyasema hayo leo Afisa Uthibiti ubora TBS, Baraka Mbajije wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS, Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika uchunguzi waliofanya wamebaini wengi wao wanaweka bidhaa nje kwenye jua ili wateja waweze kuona, sababu ambayo ni dhaifu kwani kunaweza kuhatarisha afya ya walaji.

Mbajije amesema kuwa kuweka bidhaa za vyakula nje kwenye jua inapelekea kuharibu kile chakula na ubora wa hiyo bidhaa unapungua hata kama bidhaa haijafika muda wake wa matumizi kuisha (Expire date).

Aidha amesema wazalishaji wa mafuta ya kula huongeza virutubisho vya vitamini A kuhakikisha mtumiaji anatumia mafuta yaliyobora, hivyo mafua yakiwekwa kwenye jua Vitamini A huondoka kwa haraka hivyo mtumiaji nakuwa kwenye hatari ya kutumia mafuta yasiyo salama.

Pamoja na hayo amesema chakula kilichopigwa na jua kinapoteza radha yake ya asili kwasababu ya shughuli za kemikali zilizkuwa zimefanyika katika kuandaa hicho chakula pia kuzalisha harufu ambazo hazikutarajiwa.

0/Post a Comment/Comments