WANAFUNZI MWALIMU NYERERE WATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO AMANI BAGAMOYO



 Na Mwandishi wetu


CHUO cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, wamepata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali kwa kila kushirikiana na wanafuzi wavyuo tofauti tofauti wametoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha Amani kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani.


Akizungumza na wahandishi wa habari, Bagamoyo Mkoani Pwani kwa niaba ya Mkuu wa chuo. Profesa Shadrack Mwakalila, Mwalimu Mkuu wa Idara wa Jinsia na Maendeleo  wa Chuo hicho, Dk Sara Mwakiambiki, alisema kila mwaka chuo kina kazi ya  kurudisha fadhila kwenye jamii amesema wanatoa  msaada huo kila mwaka ikiwa ni sehemu moja wapo ya kurudisha shukrani katika jamii.


"Baadhi ya wanafunzi hii ni moja ya masomo yao tunavyofanya hivi wanajifunza umuhimu wa kurudisha fadhira kwenye jamii wapo wanafunzi kama 300 walioshiriki hili." alisema Mwakiambiki


Pia Mshauri wa wanafunzi Ukwende Mkumbo, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere tumekuja Bagamoyo na Wanafunzi lengo ni kuwafariji na kuwaonyesha upendo watoto yatima, wanafunzi wanasoma kwa kodi za wananchi ni jukumu na wajibu wetu   kurudisha shukrani kwa wananchi tunachopata sio kwetu bali ni kwajamii nzima inayo tuzunguka. 


Kwa upande wa Rais wa Serikali ya Mwanafunzi wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dolson Peter Munisi, amesema kuwa tumetoa mchele, mabalo ya nguo, unga, vifaa vya shule, magodoro na mito kama sehemu ya kusaidia jamii.


"2021/2022 Ikiwa no nafasi ya kuwafariji wenye uhitaji na mazingira majumu, kwa kuwaonyesha upendo ambao wanakuwa muda mwingi wapo wenyewe niwashukuru Maso na uongozi wa chuo kuunga Mkono jambo hilo."


Alisema kilicho waamasinsha ni nguvukazi ya Rais Samia kwa kasi yake ya kufanyakazi na vijana nasisi tukiwa vijana tunaunga mkono juhudi zake anazozifanya.


Mlezi wa watoto wa kituo cha Amani, Ester Luhaa alisema tumefurahia sana kuja kwa wanafunzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere kwa mkono wa upendo waliouleta na kusaidia watoto kwenye uhitaji.


Pia ameongeza kuwa kwasasa watoto wanauhitaji wa vifaa vya shule ukizingatia ndio zimefunguliwa wanahitaji kurudisha mashuleni na kuendelea na masomo yao.

0/Post a Comment/Comments