Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bw Achiles Bufure, akizungumza na Walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Kisutu Sekindari waliotembelea Makumbusho hiyo.
Mwl Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisutu Mwl Chiku Mhado akizungumza na Wazazi na wanafunzi wa Shule hiyo, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam

Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Bi Anamary Bagenyi akiwapatia maelezo wanafaunzi wa Shule ya Sekondari Kisutu juu ya Magari yaliyotumiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisutu wakijifunza historia ya Tanzania kwenye moja ya Maonesho yaliyopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Wazazi na wafanzu wa Shule ya Sekondari Kisutu wakiwa kwenye viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam
............................
Na Catherine Ngowi
Walimu, wanafunzi na Wazazi nchini wameshauriwa kutenga muda wao
na kutembelea Makumbusho za Taifa ili waweze kujipatia maarifa zaidi ya uridhi
wa Utamaduni na Maliasili
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam Bw Achilesi Bufure kwa Wazazi, Walimu na wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Kisutu waliotembelea Makumbusho hiyo kwa lengo la Kujifunza
na kuburudika kupitia programu ya Twenzetu Makumbusho.
Bw Bufure licha ya kuupongeza Uongozi wa Shule ya Sekondari
Kisutu kwa kuitembelea Makumbusho hiyo, anatoa wito kwa wanafunzi hasa wa
kitato cha Sita kabla ya mitihani yao kwenda Makumbusho kujikumbushia kwa
vitendo yale waliofundishwa.
“Natoa wito kwa wanafunzi kujiwekea utamaduni wa kutembelea
makumbusho ili kujiongezea maarifa kwa vitendo katika masomo na kuelewa
historia na asili ya nchi kwa uzalendo wa nchi yao” Bw Bufure alisema
Licha ya kuipongeza Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, kuanzisha
program inayowapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kwa matendo, Mkuu wa Shule ya
Sekondari Kisutu Mwl Chiku Mhando amesema wanamatarajio makubwa katika ufaulu
wa wanafunzi wao baada ya kujifunza kupitia Makumbusho hiyo.
“Licha ya kuja kufanyia maafali yetu hapa ya Kidato cha Sita,
tumeona tutumie fursa hii kuona namna wanafunzi wetu wanavyo weza kufaidika na
Makumbusho hii, pamoja na wazazi wao ambao naamini wengi wao hawakufika katika
taasisi hii muhimu katika kujifunza mambo ya Historia ya nchi na uzalendo” Mwl
Mhando.
Mmoja wa Wazazi waliojumuika na wanafunzi hao ameeleza kuwa
amefurahishwa na utaratibu wa Shule hiyo ya Kisutu kwa kutumia njia nyingine ya
vitendo zaidi kufundisha wanafunzi kwa kuwa njia hiyo licha tu ya kuwafanya
waelewe haraka bali inawajenga wanafunzi kuivaa nchi yao na wao kuwa watanzania
halisi.
“Mimi kama mzazi nafarijika sana kuona watoto wetu
wanajifunza kwa vitendo mambo mbalimbali yanayohusu historia ya nchi yao, hivyo
naipongeza Makumbusho na uongozi wa shule kwa kuandaa programu hii muhimu”
aliongeza Bw Ally.
Nao Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Kisutu
Saumu Juma na Pili Mtobi Waliopata nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kufundisha
wengine kupitia maonesho ya Makumbusho, wamesema sasa watafanya mitihani yao
bila hofu na uhakika wa kufaulu ni mkubwa.
“Tunasoma vitu vingi darasani kwa nadharia, hivyo kutembelea
makumbusho ni njia ya kukamilisha kwa vitendo yale tuliyoyasoma. Hii programu
iwe endelevu kwa kuwa tunapojifunza kwa vitendo na kuona kwa macho ambapo ni
rahisi kukumbuka hata katika mitihani yetu.” Ameeleza Saumu.
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, imeamua kutoa nafasi kwa wanafunzi wa sekondari na Msingi kujifunza kwa vitendo masomo wanayofundishwa mashuleni na kisha wanafunzi hao kufundisha wengine na kuongoza wageni ndani ya Makumbusho hiyo.
Post a Comment