Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Malikale Bw
Wiliam Mwita akifungua kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho
ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar
Wajumbe wa kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Mjini Bagamoyo
Picha
ya pamoja ya wa Malikale, Makumbusho ya Taifa na Wajumbe wa kikao kazi cha
wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali
ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar
..............................
Na Sixmund J. Begashe
Makumbusho ya Taifa nchini imetakiwa kuimarisha mpango wa masoko
ili uendane na mahitaji halisi ya wadau wa ndani na nje ya nchi ili kujenga
uelewa na kuwawezesha kushiriki katika maendeleo ya kimakumbusho na Malikale
Hayo yamesemwa Mjini Bagamoyo na Bw Wiliam Mwita, kwa niaba ya
Kaimu Mkurugenzi wa Mambo ya kale nchini, Dkt Kristowaja Ntandu alipofungua
rasmi kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka
taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar kwa lengo la kuboresha
mpango huo.
Licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa mkakati wa
masoko, ameitaka Taasisi kuhakikisha mpango huo unaleta tija kwa jamii nchini
ili iweze kuifahamu vyema Makumbusho ya Taifa na kunufaika nayo
Akiwasilisha Mpango huo kwa wadau wa kikao hicho, Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga amesema kuwa Taasisi hiyo haijawahi
kuwa na mpango wa Masoko hivyo, waliona ni muhimu kufanya hivyo ili kuisogeza
Makumbusho kwa jamii.
Dkt Lwoga aliongeza kuwa, kazi ya kuandaa na kutekeleza Mpango
wa Masoko ni moja ya majukumu ambayo yamepangwa kutekelezwa kwa lengo la
kuongeza uelewa na kuvutia uwekezaji katika sekta ya makumbusho na malikale.
“Wataalamu wa mawasiliano wanaweka bayana kuwa ni vigumu kwa
jamii kushiriki kikamilifu katika jambo la maendeleo endapo hawaelewi vizuri
juu ya jambo husika, hivyo Mpango wa Masoko unalenga katika kuainisha mahitaji
ya wadau ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuendeleza na kutangaza bidhaa
za kimakumbusho na malikale” amesema Dkt Lwoga
Akizungumzia umuhimu wa Mpango wa Masoko kwa Taasisi, Dkt
Patrokl Kanje ameshauri kuwa Maafisa Mahusiano kuwa karibu na vyombo vya habari
hasa wahariri ili waweze kupata taarifa sahihi kuhusu Makumbusho ya Taifa na
malikale kwa sababu wao wao ni sehemu muhimu sana katika jamiii.
Mwisho
Post a Comment