Na Richard Mrusha
Kampuni ya wazawa jijini Dar es Salaam, ijulikanayo kwa jina la DLT CP-Tanzania, imezindua jukwaa la kimkakati la kidijitali ili kuwaunganisha watanzania kwa ujumla ikiwemo wafanyabiashara na watu wanaofanyakazi binafsi na fursa mbalimbali duniani.
Jukwaa liitwalo "GetPaid" limezunduliwa jijini Dar es Saalam Leo wakati wa sherehe zilizowaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali nchini.
"Kwa kweli, hili ni jukwaa la kidijitali la peke yake, ambalo linawaunganisha watu wa kada tofauti tofauti haswa vijaba wanao itimu elimu ya juu uku wakiwa na uhuzi wa taaluma yoyote wanaweza kutumia jukwaa hili ili kujipatia ajila hii ni njia rahisi kuliko kusuburia ajira ya serikali.alisema Mtendaji Mkuu wa DLT CP-Tanzania wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya GetPaid App.
Amesema GetPaid ni teknolojia ya kisasa, ambayo itawaunganisha watu na fursa mbalimbali kitaifa, kikanda na kidunia na itawapa unafuu wa kupata ajira popote pale hata kama ukiwa upo nyumbani unaweza kupata ajira na kuweza kufanya kazi yako na yenye malipo mazuri.
Kwa njia ya jukwaa la GetPaid, watu wa aina mbalimbali wafanyabiashara, wanaofanya kazi binafsi, watu wazima, vijana, wenye weledi na wasio na weledi - watawezeshwa kunufaika na fursa mbalimbali Afrika na nje ya Afrika.
"Jukwaa la GetPaid linawafanya waweze kunufaika na fursa mbalimbali duniani, elimu ya kidijitali na uvumbuzi. Hili linafanyika kupitia kikundi cha jumuiya, utumiaji rahisi na elimu," alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa jukwaa hilo na kuongeza kwamba "bidhaa ya GetPaid ina vitu vitatu na inawapa watumiaji (waanzilishi, wafanyabiashara na wafanyakazi binafsi vifaa na elimu wanayohitaji kuishi, kufanyakazi na ajira."
Akizungumza wakati wa uzinduzi, mtaalamu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari (ICT) Mwajuma Mbele alisema ingawa kuna ukuaji wa kasi wa uchumi wa kidijitali, bado kuna pengo kubwa linalotakiwa lijazwe, kwa vile mamilioni ya vijana katika nchi nyingi za Afrika hawana ajira.
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba pamoja na kwamba vijana wanaomaliza chuo na kuingia kwenye soko la ajira Tanzania wanaanzia 800,000 hadi 1,000,000 kila mwaka (NBS-2015), kwa wastani uchumi unatengeneza ajira zipatazo 250,000 tu kwa mwaka na asilimia 75 ya hawa vijana wanabaki bila ajira
"Hata hivyo, kutumia njia na vifaa sahihi, kama jukwaa la GetPid, nchi za Afrika zinaweza kushuhudia idadi kubwa ya vijana wakijiunga na kuingia kwenye uchumi wa kidijitali," amesema mhitimu mmoja kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Asha Mkwezu wakati wa uzinduzi wa GetPaid APP.
DLT CP-Tanzania ni kampuni iliyosajiliwa na inamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania wenye vipaji ambao wameingia kwenye "huu uchumi wa kidijitali."


Post a Comment