KATIBU MKUU NA MKURUGENZI KUTOKA OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA WAITEMBELEA OFISI ZA THRDC-ZANZIBAR




..............................

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC-Zanzibar imetembelewa na Katibu Mkuu Bw. Seif Sh. Mwinyi na Mkurugenzi Bi. Zaina Daudi kutoka Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kwa mujibu taarifa ambayo imetolewa na Afisa Habari THRDC imesema ugeni huo umekutana na kufanya mazungumzo na sekretarieti ya Mtandao wa THRDC - Zanzibar ikiongozwa na Mratibu wa THRDC- Zanzibar Bw Abdalla Abeid pamoja mmoja wa wajumbe wa bodi ya wadhamini THRDC- Zanzibar Bw. Hassan Juma  na kufanikiwa kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na mtandao na jinsi gani imejipanga katika harakati za utetezi visiwani Zanzibar.

Imeelezwa kuwa lengo la ujio huo wa Katibu mkuu na Mkurugenzi ni katika hatua za kufikia siku ya uzinduzi wa ofisi za THRDC - Zanzibar unaotarajiwa kufanyika siku za hivi karibuni vile vile kujua ofisi za mtandao zilipo na kujionea shughuli ambazo zinafanywa na mtandao katika utetezi wa Watetezi wa Haki za binadamu.

Katika kikao hicho Katibu mkuu amefurahishwa kuona kazi zinazofanywa na mtandao ni kazi ambazo zinatakiwa kufanywa na serikali isitoshe ameushukuru mtandao kuendelea kuisaidia serikali katika majukumu yake ya kujenga nchi.

Mtandao huo umekuwa ukifanya kazi zake kwa kusaidiana na tasisi mbalimbali za serikali  ikiwemo Ofisi ya Msajili Zanzibar, Mahakama, polisi, magereza, ZAECA, Tume ya kubalisha sheria, Mkurugenzi wa mashtaka, Chuo cha mafunzo, Tume ya haki za binadamu na utawala bora, Mwanasheria mkuu pamoja na  Wizara fedha na mipango..

Pia katika maongezi yake Bw. Seif ameuhimiza mtandao kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na idara maalum kwa kusaidia kutoa msaada wa kisheria, rasilimali pamoja kuwajengea uwezo (Capacity Buliding) watetezi wa haki za binadamu.

Mbali na hayo Mkurugenzi Bi. Zaina Daudi yeye ameupongeza mtandao katika shughuli zake ulizofanya kwa kusaidiana na serikali na ameuomba mtandao kutembelea ofisi za Idara za Utawala Bora ili kutambua vitengo mbalimbali ambavyo mtandao unaweza kufanya navyo kazi kwa ukaribu zaidi.

0/Post a Comment/Comments