Baadhi ya wadau ambao wameshiriki katika sherehe za utoaji wa tuzo kwa wasambazaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Limited
.................................
Na Richard Mrusha
Dkt.Majige Amesema kuwa kwakuwa kampuni ya Mafuta ya Puma Energy, ndio namba moja na yenye huduma bora hapa nchini hivyo hata kwenye uuzaji na usambazaji wa Nishati hiyo ya Gesi watakuwa namba moja Kama ilivyo kawaida yao.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ameyasema hayo wakati wa sherehe wa kutoaji tuzo hizo ambao umefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mwakilishi kutoka Hazina, wafanyabiashara pamoja na wasambaji na watoa huduma kote nchini.
"Nawapongeza wote mliopata tuzo hizi na kwakweli tunajivunia kwa huduma bora ambazo munazifanya na niwaombe mkaendelee kuitangaza, na kuilinda Puma Energy limited ili iendelee kuwa kampuni namba moja kwa ubora, "Amesema Dkt Majige
Nakuongeza kuwa hivi karibuni tunakwenda Kuaza kufanya huduma ya Biashara ya usambazaji Gesi ya majumbani kwani tayari Bodi imeshakaa na kupitisha hilo hivyo matarajio yangu nikuona tunaendelea kuwa namba moja kwa ubora wa huduma zetu hivyo nawapongeza nyote kwa kazi nzuri mnayofanya. "amesisitiza Majige
Pia akizungumzia Kampuni hiyo amesema kuwa wameendelea kuwa namba moja kwani kila kituo ambacho utakwenda utakuta huduma hiyo ya mafuta na hivi sasa wameongeza vituo kutoka 52 vya awali nakufikia vituo 80 lakini lengo nikuona hadi kufikia mwaka 2025 wanakuwa na vituo 150 na sio 100.
"Niombe Menejimenti ya Kampuni hii ya Puma kwamba hadi kufikia mwaka 2025 muwe mmeongeza vituo hadi kufikia 150 na sio 100 kama mlivyokuwa mmepanga mimi naamini tunaouwezo wa kufikia vituo 150 hivyo tujielekeze huko kwani uwezo upo na muhakikishe vituo hivyo vinafikia. "Amesema Dkt. Majige
Dkt Majige amewaeleza wadau hao na kuwakumbusha Kuwa Puma ni kampuni kubwa hivyo waendelee kuilinda na kuhakikisha mafuta yanakuwa salama lakini pia ameitaka menejimenti kuweka mkakati wa kuaziasha vituo vijijini ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi.
Amemaliza kwa kuendelea kuwakumbusha watoa huduma kutumia maneno mazuri kwa wateja kwani hiyo ndio silaha ya Puma energy kuendelea kuwa namba Moja na kwakufanya hivyo kutawafanya wateja kufurahia huduma zao Kama ilivyokawaida.
Awali wakati akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Limited ,Tanzania Dominic Dhanah Amesema Kampuni hiyo ndio inayoongoza nchini na inashika namba moja kwa ubora.
Amesema kuwa namba moja ni kazi kubwa sana lakini wataendelea kuwekeza nakwamba hadi kufikia sasa Puma inavituo 80 kutoka vituo 52 vilivyokuwepo hapo mwanzo na lengo nikufikisha vituo 100 kufikia mwaka 2025.
"Ndugu Mgeni rasmi kampuni imeendelea kuwa wabunifu na tumeongeza huduma nyingine ya vilainishi vya kwenye magari na mapema mwaka huu tunatarajia kuzindua nishati ya gesi ya majumbani ambayo itakuwa inapatikana kwenye vituo vyetu vyote na hakuna shaka kwamba itapokelewa vizuri. "Amesema Dhanah
Pia amewapongeza watoa huduma wote wa Puma energy nakusema kwamba wao ndio chachu ya mafanikio ya kampuni hiyo huku akiwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi na katika tuzo hizo kituo cha mafuta kutoka Arusha cetral station kimefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa uuzaji wa mafuta na hiyo ni mwaka wa pili mfululizo.
Katika tuzo hizo washiriki walifanikiwa kupata tuzo ya vikombe
na pesa taslimu sh.laki mbili na nusu 250,000 kama motisha na kuwapa hamasa ya
kuendelea kufanya vizuri zaidi.
Post a Comment