Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe David Silinde (MB) akiweka sahihi kwenye Bango lenye vielelezo vya mradi wa Maboresho ya Makumbusho ya Majimaji, kama sehemu ya uzinduzi rasmi wa mradi huo.
Maandamano yakiingia Makumbusho ya Majimaji Sogea kwenye uzinduzi wa Mradi wa kuboresha Makumbusho ya Majimaji Songea na kilele cha Tamasha la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni, Songea
Bango lenye vielelezo vya mradi wa Maboresho ya Makumbusho ya MajiMaji
Na Sixmund J. Begashe
Serikali imeipatia Makumbusho ya MajiMaji
jumla ya Shilingi Milioni Sitini (60,000,000/) ili kutekeleza mradi wa
uboreshaji wa Makumbusho ya Majimaji Songea ambao unatarijiwa kuongeza ufanisi
zaidi katika kutoa huduma kwa wageni watakao itembelea Makumbusho hiyo pamoja
na kazi ya uhifadhi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa Bi Joyce Mkinga kwenye uzinduzi wa mradio huo ulio enda
sambamba na Tamasha la kumbukizi ya Mashujaa wa Vita ya Maji Maji na Utalii wa
Utamaduni kwa mwaka 2022
Bi Mkinga licha ya kuishukuru serikali
chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kuishika mkono Makumbusho ya Taifa, amesema mradi huo ni sehemu ya
miradi 15 inayotekelezwa na Taasisi hiyo chini ya ufadhili wa Miradi ya Kuinua
Ustawi wa Nchi na Mapambano dhidi ya UVIKO -19
Akizindua mradi huo, Naibu Waziri wa
Tamisemi Mhe Divid Silinde (MB) licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa chini
ya Mkurugenzi Mkuu, Dkt Noel Lwoga kwa kazi nzuri zinazofanyika ameitaka
Taasisi hiyo kuhakikisha inatumia fedha za mradi huo kama ilivvyo kusudiwa na
si vinginevyo
”Natambua Wizara inafuatilia kwa ukaribu
utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa na Makumbusho ya Taifa ili
kuhakikisha kuwa lengo la Serikali linafikiwa. Kutokana na juhudi hizi sina
shaka kwamba Miradi hii niliyoizundua leo itatekelezwa kwa weledi na ufanisi
kwa kuzingatia taratibu zote za matumizi ya fedha za umma” Mhe Silinde
Awali Mratibu wa Mradi huo ambaye pia ni
Muhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji Songea, Bw Baltazari Nyamusya alieleza kuwa
fedha hizo zitakwenda kuboresha kumbi za maonyesho, stoo kwa ajili ya uhifadhi
wa mikusanyo, na ujenzi wa choo utakao saidia kuweka mazingira mazuri kwa
wageni watakao itembelea Makumbusho hiyo.
Sanjari na Uzinduzi wa mradi huo, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe David Silinde (MB) alifunga rasmi Tamasha la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni.
Post a Comment