
Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Masanja Kadogosa akimueleza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (aliuevaa shati jeupe) maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa Dar es salaam-SGR.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa Dar es salaam-SGR
............................
NA MUSSA KHALID
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame
Mbarawa ameuagiza Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha
wanasimamia ujenzi wa Jengo la Stesheni ya Reli ya Kisasa Dar es salaam-SGR
kukamilika kwa wakati kabla ya mwezi wanne mwaka huu.
Waziri Prof.Mbarawa amesema hayo leo jijini
Dar es salaam wakati akifanya ziara ya kukagua maendeleo ya Shesheni hiyo akiwa
ameambata na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Masanja Kadogosa pamoja na
wafanyakazi wa shirika hilo.
Aidha Prof Mbarawa ametoa maelekezo kuwa
jengo hilo limalizike kwa haraka lakini
pia litakapoanza kutumika liwekewe usimamizi mzuri ili lindelee kuwa katika
ubora wake.
Amesema wakati umefika jengo hilo liweze
kumalizika na sio kuahidi kili wakati hivyo mpaka mwezi wa nne mwaka huu ni
vyema likakamilika.
Amesema pia Jengo hilo lifanyiwe ukarabati wa
mara kwa mara ili liweze kukaa kwa muda mrefu na na hivyo kuonekana kuwa la
mfano kwa wageni mbalimbali pamoja na wananchi pindi wanapolitembelea.
‘Hili jengo ni zuri sana kwani limejengwa kwa
miundombinu mizuri hivyo ni lazima tuwe na utamaduni wa kuja kulisimamia
vinginvyo miaka miwili au mitatu litakuwa halitamaniki lazima
tubadilike’amesema Prof Mbarawa
Hata hivyo amewataka TRC kubadilika katika utoaji wa huduma wa SGR tofauti na treni ya zamani ili watu waone utofauti wa kuwa treni hiyo ni ya kisasa kwani kufanya hivyo watapata heshima kubwa kwa watanzania.
Post a Comment