TBS YATOA NENO WASAFIRISHAJI BIDHAA NJE YA NCHI

 =

Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Hassan Juma wakati akizungumza na wanahabari akielezea huduma inayotolewa na TBS


Ibrahim Feruzi kutoka kitengo cha Upimaji wa Sampuli  kwa Hiari (TT) akizungumza na waandishi wa habari akielezea umuhimu wa kulitumia dawati la TT.

............................. 

NA MUSSA KHALID

Shirika la Viwango Tanzania –TBS limesema limeanzisha kituo cha Taarifa kwa bidhaa zinazosafirishwa kwenda mataifa mbalimbali ili kutoa usaidizi kwa wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zilizokidhi viwango vya nchi husika.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Hassan Juma wakati akizungumza na wanahabari akielezea huduma inayotolewa na TBS ikiwemo ya kutoa ushauri kwa wasafirishaji wa bidhaa kwenda nje ya nchi.

Hassan amesema kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki bidhaa ambayo imethibitishwa  na TBS huwa haina kipingamizi lakini zinazokwenda nje huwa wanazikagua kabla ya kwenda nje sambamba na utoaji wa cheti.

‘Kwa bidhaa zinazokwenda nje ya jumuiya ya Afrika Mashariki huwa tunawapa taarifa ya bidhaa zinavyokwenda huwa tunakagua ubora wake kabla ya kuisafirisha na pia itatolewa cheti cha uthibiti’amesema Hassan

Kwa upande wake Ibrahim Feruzi kutoka kitengo cha Upimaji wa Sampuli  kwa Hiari (TT) ameelezea umuhimu wa kulitumia dawati la TT kuwa ni pamoja na kufanya uhakiki wa bidhaa kwa wajasiriamali wanaoanza biashara kujihakikishia wanapata leseni baada ya kujihakikishia  ubora wa bidhaa zao.

‘Upimaji wa hiari unasaidia wanaohitaji huduma za upimaji kuhakiki ubora wa bidhaa wanazokuja kuzipima kwa kuhakikisha uimara wa miundombinu ya miradi mikubwa ya kimkakati lakini usalama kwa ajili ya watumiaji’amesema Feruzi

Aidha ametoa wito kwa wananchi wote kufahamu kwamba TBS kuna dawati la upimaji wa sampuli kwa hiari hivyo wanauhuru wa fursa ya kulitumia dawati hilo kwa manufaa yao kujihakikisha ubora wa bidhaa wanazonunua na wanazotarati kwenda kuzitumia katika ujenzi na matumizi ya kila siku.

Hata hivyo Feruzi amesema ripoti za wateja ambazo wanazipokea katika dawati lao zinatoka ndani ya siku 7 hadi 14 ikitegemeana na aina ya sampuli na maabara inapopelekwa .

0/Post a Comment/Comments