TMA: MWAKA 2021 ULIKUWA NA MATUKIO YA HALI MBAYA YA HEWA.


 
Mkurugenzi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi,
...............................................

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania –TMA imesema kuwa mwaka 2021 ulikuwa na matukio ya hali mbaya ya hewa, hususan mvua kubwa, mafuriko, vipindi virefu vya hali ya ukavu, upepo mkali na hali ya joto kali, ambavyo viliathiri maisha kwa kiasi kikubwa. 

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi,wakati akitoa taarifa ya klimatolojia hali ya hewa kwa mwaka 2021 kwa Tanzania. 

Dkt Kijazi amesema kuwa kuwa mwaka 2021 ulikuwa na joto la juu ya wastani wa muda mrefu (1981-2010) kwa kiwango cha nyuzi joto 0.50C ambapo hali hiyo inaweza ikawa imeathiri afya za binadamu na wanyama, uzalishaji, usindikaji na uhifadhi wa vyakula, na Mwezi Novemba 2021 ulivunja rekodi ya kuwa na joto kali zaidi ikilinganishwa na miezi ya Novemba ya miaka ya nyuma tangu 1970. 

“Kipindi cha ukavu cha muda mrefu kilitokea katika miezi ya Oktoba na Disemba 2021 na kusababisha athari kubwa kwa jamii na uchumi hasa jamii za wafugaji ambapo idadi kubwa ya mifugo ilikufa kwa kukosa malisho na maji katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Manyara na Pwani”. Alisema Dkt Kijazi. 

Aidha Dkt. Kijazi amesema kipindi cha ukavu cha muda mrefu kilitokea katika miezi ya Oktoba na Disemba 2021 na kusababisha athari kubwa kwa jamii na uchumi hasa jamii za wafugaji ambapo idadi kubwa ya mifugo ilikufa kwa kukosa malisho na maji katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Manyara na Pwani. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Kijazi alitoa taarifa ya tathimini ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa (IPCC WGII report) iliyotolewa na Jopo la Kiserikali la Tathmni ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) ikieleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanayojumuisha kuongezeka kwa idadi na ukubwa wa matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo ukame na mvua kubwa pamoja na ongezeko la joto ambalo linatarajiwa kufikia nyuzi joto 1.50C ifikapo mwaka 2040 endapo hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa hazitachukuliwa hasa kwa nchi zinazozalisha gesi hiyo kwa wingi duniani na yameendelea kusababisha athari na madhara makubwa zaidi kwa jamii, viumbe hai na mfumo mzima  wa ikolojia.

“Uwezo wa kuhimili changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa utakuwa mashakani zaidi endapo ongezeko la joto litazidi nyuzi joto 1.50C”. Alieleza Dkt. Kijazi wakati akiwasilisha masuala yaliyoainishwa katika taarifa ya Jopo hilo la Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi. Taarifa hiyo ya jopo la kisayansi inapatikana katika tovuti ya IPCC.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya huduma za hali ya hewa Dkt.Ladislaus Chang'a ameeleza mifumo mbalimbali ya hali ya hewa mwaka 2021 ambapo amesema kuwa wastani joto katika sehemu mbali nchini linaendelea kuongezeka kwa kasi

0/Post a Comment/Comments