WAJUMBE WAJIFUNGIA KUSUKA MITAALA TANZANIA



Serikali imewataka  wataalamu wanaoandaa muundo wa mitaala nchini, kuhakikisha wanakidhi matamanio ya Watanzania ya kuwa na mitaala mipya ya Elimu kuanzia ngazi ya  Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu.


Hayo yameelezwa leo tarehe 23/03/2022 na Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo katika mazungumzo yake na wataalamu wanaoendelea na kazi ya uandaaji wa muundo wa mtaala.


"Serikali inawategemea mmalize kazi hii kwa wakati na weledi na mitaala mipya ianze kutumika kama ilivyokusudiwa" amesema Prof.Nombo 


Kazi ya uandaaji wa muundo wa mitaala inaendelea kufanyika Mjini Morogoro kuanzia tarehe 21 machi 2022, ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati wataalamu (technical commitee) inayosimamia kazi ya maboresho ya Mitaala Pro.Makenya Maboko pamoja na wajumbe kutoka vyuo vikuu,Wizara,TET, TEZ na wataalam kutoka sekta binafsi.





0/Post a Comment/Comments