Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika,Al Ahly wamefanikiwa kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuilazimisha sare ya 1-1 Raja Casablanca ya Morocco kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya michuano hiyo uliochezwa kwenye dimba la Stade Mohamed V ambapo ni nyumbani kwa Raja Casablanca hivyo Al Ahly wamefuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2 ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Al Salam Stadium ulimalizika kwa Al Ahly kushinda 2-1.
Goli la Al Ahly limefungwa na Mohammed Abdulmonem wakati lile la Raja Casablanca likifungwa na Fabrice Ngoma na Al Ahly watapambana na Entente Sportive Setif ya Algeria kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.
#Timesfm

Post a Comment