NA Richard Mrusha.
Meli hiyo inayojulikana kwa jina la Frotier ace imewasili Leo kwenye Bandari ya Dar es salaam ikitokea jampani imetembea baharini kwa mda wa siku 19 Badala ya siku 40, Kama ambavyo ilikuwa itembee kwa mda wa siku 40 baharini
Hayo yamesemwa na Waziri wa ujenzi na uchukuzi profesa Makame Mbalawa Wakati wakupokea meli hiyo ilipowasili bandari pamoja na viongozi wengine wa mamlaka ya bandari Tanzania (TPA)
Mbalawa amesema ameiagiza mamlaka ya bandari Tanzania (TPA)
kuyaondoa makasha (makontena )yote yanayokaa kwa Muda mrefu kwenye bandari hiyo yatolewa kwani banadri sio sehemu ya kuhifadhia makontena Bali ni sehemu ya kushushia mizigo.
Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuboresha Kitengo Cha Masoko kwa kutangaza Huduma Bora zinazotolewa na kuhamasisha watu Ili waweze kutumia bandari hiyo.
Na kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania( TPA) Mhandisi Erick Hamis
amesema Magari elfu Moja sawa na Asilimia 27 yatasalia Nchini na
Asilimia 73 yatakwenda nje ya Nchi,na nchi hizo ni sudani ya Kusini, Zimbabwe, na msumbiji kwasababu nchi hizo zinazotumia Bandari ya Dar es salaam kutolea magari yao.
amesema tarehe 5 Hadi Saba Mwezi huu Banadari hiyo ilipokea meli mbili zikiwa na magari elfu nne ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya kuaminika kwa Bandari ya Tanzania.
Hamis amesema ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassan kwa kazi kubwa inayofanya hi vyo amesema bandari ya dar es salaam ni bandari salama hivyo watu nchi jirani waendelee kuitumia.


Post a Comment