ESPERANCE YATUPWA NJE KWENYE LIGI YA MABINGWA

 



Entente Sportive Setif imefuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya kuichapa Esperance Sportive De Tunis 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya michuano hiyo, uliochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Esperance, Stade Olympique Hammadi Agrebi na hivyo Setif wanafuzu kwa ushindi wa jumla wa 1-0 ambapo mchezo wa kwanza ulimalizika kwa suluhu ya 0-0.


Goli la ES Setif limefungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Abdulmoumene Djabou raia wa Algeria, sasa timu hiyo itapambana na mabingwa watetezi Al Ahly kwenye mchezo wa nusu fainali.




0/Post a Comment/Comments