NA SALYM BITCHUKA.
Kampuni ya Itel Tanzania imewataka Wadau
wa elimu nchini kuhamasika kuunga mkono jitihada za serikali katika
kuchangia maendeleo ya elimu nchini
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam wakati kampuni
hiyo ya Itel Tanzania ilipokabidhi msaada vifaa vya shule kwa
wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu au famili zenye kipato
cha chini ya mstari wanaosoma katika shule ya msingi Ubungo NHC jijini hapa
kupitia kampeni yao ya CSR.
Akizungumza katika makabidhiano hayo meneja mahusiano Itel Tanzania
Fernando Wolle amesema kwa kutambua watoto ni hazina ya taifa
lijalo hivyo itel kwa kutumia kauli mbiu yao ya "Enjoy Better Life"
Wanahakikisha wanatengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kutimiza azma ya
kuwasaidia watoto kufurahia maisha bora.
‘Pia tumeanzisha mradi wa maktaba unaojulikana kama ‘Wandering Libraries
Project’tangu 2021 na huu utakuwa mradi wa muda mrefu wa CSR wa Itel lengo ni
kuchangia maktaba ndogo zaidi ya 10,000 kote barani Afrika katika miaka 3
ijayo.’amesema Wolle
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo NHC Paulo Mdachi
ameshukuru Kampuni ya Itel Tanzani kwa msaada huo huku akiwataka
wadau wengine wa elimu juiga mfano wa Itel mobile limited.
Msaada huo uliotolewa na Kampuni ya Itel Tanzani kwa wanafunzi hao ni pamoja vitabu vya kiada 217 kwa masomo ya sayansi, Hesabu na Kiingereza kwa darasa la tatu la nne na la tano, Shelfu ishirini, Kalamu na mabegi ya shule vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano.




Post a Comment