Liverpool imetanguliza mguu mmoja kwenye nusu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Villarreal goli 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya uliochezwa kwenye uwanja wa Anfield.
Magoli ya Liverpool yamefungwa na Sadio Mane pamoja na goli la kujifunga la mlinzi wa kushoto wa Villarreal, Pervis Estupinan.
Mchezo wa mkondo wa pili unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Villarreal wa Estadio de la Ceramica jumanne ijayo.
#TimesFMDigital

Post a Comment