Manchester City imepata ushindi wa goli 4-3 mbele ya Real Madrid kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya uliochezwa kwenye uwanja wa Etihad Stadium.
Magoli ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne, Bernado Silva, Gabriel Jesus na Phil Foden, kwa upande wa Real Madrid magoli yao yamefungwa na Karim Benzema aliyefunga mara mbili pamoja na Vinicius de Oliveira "Vinicius jr"
Mchezo wa mkondo wa pili unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Real Madrid, Estadio Santiago Bernabeu siku ya jumatano ya wiki ijayo.
#TimesFMDigital

Post a Comment