MOI NA RAMAIAH YAENDESHA UCHUNGUZI BILA KUFUNGUA FUVU KWA MBINU ZA KISASA



 Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Ramaiah India imeendesha kambi maalum ya uchunguzi na tiba ya mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu kwa mbinu za kisasa. 


Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema zaidi ya wagonjwa 160 wameshapatiwa huduma katika maabara hiyo toka ilipoanza kazi mwaka 2021.Maabara hiyo imejengwa na Serikali kwa zaidi ya Tsh Bilioni 7.9.


“Hivi karibuni tulianzisha ushirikiano na wenzetu hawa hospitali ya Ramaiah India ili tushirikane katika kuboresha huduma zetu za uchunguzi na tiba ya Ubongo hapa nchini, sasa ndio wamekuja na wamewahudumia wagonjwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu wetu ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kisasa za upasuaji”. Alisema Dkt. Boniface


Dkt. Boniface amesema hii ni sehemu ya mkakati wa MOI wa kuhakikisha huduma zote za kibingwa za ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zinapatikana hapa nchini ili kuiondolea mzigo mkubwa Serikali wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kutafuta matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini.


Kwaupande wake daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo kutoka Hospitali ya Ramaia India Dkt. Sunil Valentine Furtado amesema ujio wao umetokana na majadiliano ambayo yalifanyika baina yao na uongozi wa MOI ambapo ushirikiano baina ya Taasisi hizi unalenga kuboresha huduma kwa wagonjwa, kubadilishana uzoefu na mafunzo.

0/Post a Comment/Comments