PETRO ATLETICO LUANDA YAITUPA NJE MAMELODI

 



Petro Atletico ya Angola imeing'oa Mamelodi Sundowns ya Afrika ya Kusini kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kuilazimisha sare ya 1-1, kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya michuano uliofanyika kwenye uwanja wa Lucas Masterpiece Moripe Stadium


Kwa maana hiyo Petro Atletico Luanda wanafuzu nusu fainali ya michuano hiyo kwa jumla ya goli 3-2, ambapo mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Petro Atletico Luanda ilishinda 2-1 wakiwa nyumbani kwao kwenye dimba la Estadio 11 de Novembro


Goli la Mamelodi limefungwa na Brian Onyango wakati la Petro Atletico limefungwa naTiago Azulao, na sasa Petro wanasubiri mshindi baina ya Waydad Casablanca dhidi ya CR Belouizdad unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 7 usiku wa leo kwenye nusu fainali.






#TimesFMDigital

0/Post a Comment/Comments