Mwenyekiti wa Taasisi ya kuandaa Tamasha la kitalii la "FESTAC AFRICA" nchini Tanzania Hassan Ali Mzee akizungumza na waandishi Wahabari jijini Dar es salaam mara baada ya kutambulisha rasmi Tamasha hilo lenye lengo la kukuza utalii nchini.
****************************
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
TAASISI ya kizanzibar ya kuandaa safari za kitalii (ZATO) inatarajia kuandaa tamasha lenye lengo la kukuza na kuendeleza utalii wa Tanzania Bara na visiwani Zanzibar.
Tamasha hilo litashirikisha nchi za Afrika inayotarajiwa kufanyika Mei 23 hadi Mei 29 mwaka huu visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Michuzi Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa taasisi hiyo ya (ZATO )Hassan Ali Mzee amesema tamasha hilo litashirikisha michezo, burudani, mitindo na biashara mbalimbali.
“Nchi 54 kutoka Afrika zitashiriki kwa ajili ya kudumisha mila na desturi za waafrika pia kuona mambo ya kale ambayo yanapatikana Zanzibar".
Aidha Mwenyekiti huyo aliongezea kuwa tamasha hilo litahudhuriwa na wachezaji mashuhuli wa mchezo wa gofu na soka la ufukweni kwa wanawake na wataonyeshana uwezo.
“Wachezaji mashuhuli kutoka Afrika wataonyesha viwango katika mchezo wa gofu, pia bado tunapokea wachezaji ambao wanatamani kuonyesha uwezo wao."
Mwenyekiti wa tamasha hilo kutoka nchi ya Nigeria, Yinka Abioye alieleza zaidi kuwa tamasha hilo litafanyika kwa miaka mitano hapa nchini baadae litafanyika nchi nyingine.
Abioye amesema katika tamasha hilo litaibua vipaji vya vijana katika sekta ya muziki na kuviendeleza.
“Kutakuwa na viongozi mbalimbali ambao watatoa mada katika tamasha hilo akiwemo Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, AshaRose Migiro na Rais Mstaafu wa Botswana."

Post a Comment