Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania-TMA Dkt Agnes Kijazi akizungumza na wananahabri jijini Dar es salaam akielezea mwenendo wa athari za mabadiliko ya Tabia nchi katika mifumo ya hali ya hewa na mwenendo wa mvua za masika mwaka huu.
Mratibu wa maafa Ofisi ya waziri Mkuu Idara ya usimamizi wa maafa Khowe Malegeri akizungumza nanma ofisi hiyo itakavyokabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza.
Mdau Katika Sekta Ya Kilimo Juma Makandi
akielezea jinsi watakavyo utumia utabiri huo ambao umetolewa na mamlaka ya hali
ya hewa.
................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania-TMA
imewashauri wakulima katika kipindi kilichosalia cha msimu wa masika mwaka
huu,kuzingatia matumizi ya mbinu na teknolojia za kilimo himilivu za kuhifadhi
maji na unyevunyevu wa udongo pamoja na kuzingatia maelekezo ya maafisa ugani
kwenye maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi wakati akizungumzia mwenendo wa athari
za mabadiliko ya Tabia nchi katika mifumo ya hali ya hewa na mwenendo wa mvua
za masika mwaka huu ambapo amesema mvua inatarajiwa kuwa ya chini ya wastani
hadi wastani.
Dkt Kijazi amesema kutokana na kujitokeza kwa
matukio ya vimbunga katika bahari ya Hindi eneo la Rasi ya Msumbiji kusini
kumesababisha kuwepo na vipindi virefu vya ukavu vilivyojitokeza kipindi cha
mwezi machi hususani kwa maeneo ya pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu
Kaskazini Mashariki ambapo maeneo hayo yamepata mvua chache.
‘Vilevile yamejitokeza mabadiliko ya muda
mfupi ya joto la bahari katika eneo la Pwani ya Afrika Mashariki na eneo la
mashariki mwa bahari ya Hindi.Mabadiliko hayo ya muda mfupi ya joto la bahari
ambayo ni nadra kutokea kutokana na tabia ya bahari kutunza joto au baridi kwa
muda mrefu yamesababishwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi’amesema Dkt
Kijazi
Amesema mwenendo huo wa vimbunga na
mabadiliko katika joto la bahari vimechangia ukandamvua kuendelea kusalia
katika maeneo ya kusini mwa nchi ambapo kwa kawaida katika kipindi cha mwanzoni
mwa mwezi Machi huanza kuelekea maeneo ya Kaskazini mwa nchi.
Kuhusu athari zinazoweza zinazotarajiwa Dkt
Kijazi amesema kunatarajiwa kuwepo kwa upungufu wa unyevu katika udongo ambapo
hali hiyo inaweza kuathiri ukuaji wa mazao,upatikanaji wa malisho kwa ajili ya
mifugo na wanyamapori pia upo uwezekano wa kuongezeka kwa athari za magonjwa ya
kuambukiza,hususani yatokanayo na maji yasiyosalama.
Kwa upande wake Mratibu wa maafa Ofisi ya
waziri Mkuu Idara ya usimamizi wa maafa Khowe Malegeri amezielekeza sekta zote
zinazohusiana na kilimo mifugo na miundombinu kuchukua hatua stahiki ili
kurejesha hali inayopelekea kuwepo kwa upungufu wa chakula na kudhurika kwa
mifugo.
Juma Makandi ni mdau katika sekta ya Kilimo
amesema watahakikisha wanafanyia utekelezaji taarifa hizo ambazo zimetolewa na
TMA huku akiwashauri wakulima kutumia njia himilivu zinazoweza kutunza unyevu
na maji.
Hata hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kuzingatia taarifa za hali ya hewa zilizotolewa na zitakazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ikiwa ni pamoja na kutafuta,kupata na kufuata ushauri wa wataalamu katika sekta husika ili kuweza kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.




Post a Comment