Na.Dominic Haule.
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo imesema kuwa imedhamilia kufanya Mabadiliko ya kiutendaji wa Majukumu yao ikiwemo Kubadilisha mitazamo na fikra ya Ufanyaji kazi katika Sekta Mifugo ili kuhakikisha Sekta hiyo inakuwa mfano katika Utendaji wao hapa nchini.
Hayo amesema Jijini Dar es salaam na BwanaTixon Nzunda Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo Wakati wakufunga Mafunzo ya Waalaamu wa Afya ya Mifugo.
Hatahivyo amesema kuwa Kupitia Mafunzo hayo yata watalaam kuwasadia wao Kubadilisha fikra zao Kubadilisha wafungaji kujitambua juu ya Ufugaji Bora wa Mifugo yao .
Aidha Amewataka wakufunzi hao wa Mifugo hao kuendelea kushirikiana na wafungaji katika Ufanyaji kazi zao ili kuhakikisha wana leta matokeo chanya.
Kwa upande wake mtaalamu mnyororo wa thamani shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa FAO Dkt. Moses Olenesele amesema Tanzania kumekuwa na changamoto ya utoaji taarifa juu mienenendo ya magonjwa ya mifugo hivyo utoaji mafunzo kwa wataalamu hao mwanzo wa suluhu ya changamoto hizo.
nao baadhi ya wataalamu ambao ni wahitimu wa mafunzo hayo wamesema katika mafunzo hayo wameweza kufanya tafiti ambazo zimewasaidia kuboresha kazi zao katika utambuzi wa magonjwa ya mifugo pamoja na kuwa na mipango mkakati wa kudhibit magonjwa ya mifugo.
Mafunzo hayo yametolewa kwa wataalamu wa afya ya mifugo kutoka ngazi ya serikali za mtaa, wilaya na mikoa lengo ni kuboresha sekta ya mifugo katika kukuza uchumi wa nchi.




Post a Comment