Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe akitolea tamko malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake na wakazi wa Nzasa kuhusu adha wanayoipata kuhusu kelele zinazozalishwa na muziki katika bar na Klabu.
Mwenyekiti wa mtaa wa Chuo kikuu Nzasa Dkt. Edwinus Lyaya akielezea adha wanayoipata kutokana na baadhi ua klabu na bar zilizopo katika maeneo yao
..........................
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Godwin Gondwe amewataka wamiliki wa Bar na Klabu kuendesha biashara zao kwa kufuata sheria, Taratibu , Kanuni na Miongozi na kuachana na kero ya kuzalisha Kelele kupita Kiwango.
Hayo yanajiri mara baada ya Wakazi wa Kata ya Kijitonyama jijini hapa kuwasilisha malalamiko yao kwa mkuu huyo wa Wilaya kuhusu baadhi ya Bar na Klabu kuzalisha Kelele zinazotokana na upigwaji wa Muziki kwa sauti ya juu pamoja vitendo vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wateja maeneo hayo.
Akizungumzia malalamiko hayo Ijumaa Mei 13, 2022 Mkuu wa Wilaya Godwin Gondwe amekiri kuwepo kwa tatizo la Upigwaji wa Muziki bila kufuata sheria zilizopo huku akiahidi kuanzisha operesheni maalum itakayoendana na utolewa wa elimu kwa Wananchi na Wamiliki wa Bar na Klabu ili kuondokana na adha hiyo.
"Hili ni suala ambalo lipo na lazima tukae na tuone ni kwa namna gani tunaweza kulimaliza ila ni lazima wamiliki wa Klabu na bar wasizidishe kupiga muziki zaidi ya desibeli 40 na siku za kazi wafunge saa tano kama vibali vyao vinavyowataka"amesema dc Godwin Gondwe.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa eneo hilo la Kijitonyama akiwemo mjumbe wa nyumba Hamsini Mariam Sepetu pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Chuo Kikuu Nzasa Dkt Edwinus Lyaya wamesema kwa pamoja wamesema wamekuwa wakikumbana na adha kubwa katika makazi hayo ikiwemo kelele zinazosababishwa na Muziki ,utovu wa nidhamu kwa wateja wa maeneo hayo ya starehe huku wakitaka kuwekwe taratibu za kudumu katika kudhibiti hilo.
"Kiukweli hatuchukii wafanyabiashra ila Wateja wao na upiigaji wa muziki kwa sauti kubwa, wanapaki magari hadi kwenye mageti yetu,kondomu chupi zikulitupwa hovyo yaani imekuwa imekuwa ni kero iliyopitiliza" amesema Mariam Sepetu.
Imeelezwa kuwa Katika Vilabu na Bar vilivyopo maeneo ya Wilaya ya Kinondoni vimekuwa havifuati sheria za kuzingatia upigwaji wa muziki kwa nyakati zote.


Post a Comment