....................
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Almasi Nyangassa amewataka Wamiliki wa wa Daladala Kigamboni kuwasilisha changamoto zinazowakabili mapema ili zifanyiwe kazi na kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukua hatua ya kusitisha huduma kwa wwananchi.
Alisema hayo katika kikao Maalum kufuatia mgomo wa daladala ambacho kilishirikisha wamiliki wa daladala na uongozi wa LATRA na Mkuu wa Wilaya mwenyewe na kutatua mgogoro huo.
Pamoja na kutatua mgomo wa daladala, mkutano huo pia umejadili pia changamoto mbalimbali zinazowakabili wamiliki wa daladala
Kwa upande wao baada ya mazungumzo na ufafanuzi wa mambo kadhaa, wamiliki wa daladala wameahidi kushirikiana na serikali ya Wilaya katika kuhakikisha huduma ya usafirishaji abiria inafanyika kwa ufanisi


Post a Comment