Dkt.MPAMGO AMEWAHASA WATAFITI TANZANIA KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA AMBAZO ZITALETA SULUHISHO KWA JAMII.

 


Na Richard Mrusha


Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Philip Mpango amewataka watafiti wa Magonjwa Mbalimbali kuhakikisha wanafanya tafiti zitakazoleta suluhisho Kwa Jamii kuhusu changamoto Mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza.


Dr.Mpango ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la  kisayansi la 31 lililoandaliwa na  NIMR,ambapo limewakutanisha Watafiti Mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi ikiwa lengo ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi.


 amesema kwamba tafiti zinazofanywa na Watafiti zinaisadia Serikali kuchukua maamuzi ya kisera katika kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayojitokeza Kwa Jamii akitolea mfano  magonjwa ya mripuko, na magonjwa ya kuambukiza kama vile janga la UVICO 19 lililosumbua Dunia nakusabisha vifo vya watu na uchumi kuporomoka.


Katika hatua nyingine Makamu huyo wa rais  Dr.Philip Mpango amekabidhi tuzo za NIMR Kwa Watafiti sita,pamoja nakuwazawadia shilingi milioni moja Kwa kila mmoja wao, nakutumia fursa hiyo kumuagiza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuanzisha tuzo ya watafiti vijana itakayokuwa ikitolewa kila mwaka na Wizara hiyo ikiwa lengo ni kufanya motisha Kwa watafiti hao.


Serikali kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameiagiza NIMR kufanya pia tafiti za tiba  asili  kwani asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia tiba hizo pasipokua na elimu  yakufahamu kama zinaweza kuwa na madhara ya sumu nakusababisha athari zakiafya.


Hata hivyo amesema Kwa mwaka 2018 wasichana walio na umri wa kuanzia miaka 12 hadi 14 walikuwa wanachanjwa chanjo ya  Saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi,ambapo ilikua dozi mbili nakwamba walichanjwa  asilimia 70 ya wasichana  katika awamu ya kwanza lakini awamu ya pili  wakarudi wasichana wachache kuchanja chanjo hiyo, hali ambayo iliifanya  NIMR ifanye utafiti wa chanjo hiyo na kubaini kua chanjo moja waliopatiwa  inatosha hivyo kuanzia tarehe 1 mwezi wa Saba mwaka huu  itaanza kutolewa chanjo moja pekee ya Saratani ya shingo ya uzazi


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa na Tiba ( NIMR) Prof.Yunus Mgaya amemuhakikishia Makamu wa rais Dr.Philip Mpango pamoja na Waziri wa afya kuwa utafiti wa chanjo ya Ugonjwa wa UVIKO 19 unaendelea kufanyiwa nakwamba majibu ya utafiti huo yatakamilika mwishoni mwa mwaka huu.


Aidha amesema Kuanzia mwezi wa kumi na mbili walianza kufanya tafiti ya chanjo za corona ,kuna dozi za kutosha za chanjo ya corona kilichobaki nikuwandiakisha wananchi kwenye vituo  vya Dar es salaam na Mbeya ,hivyo wanafanya tafiti hizi Kwa awamu,watatoa majibu ya tafiti mwisho wa mwaka huu


Kongamano hilo linatarajiwa kufikia kilele Mei 19 mwaka limebeba ujume usemao" Ushiriki wa sekta mbalimbali katika afya kufikia huduma ya afya wote" ambapo limehudhuliwa na wataam mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi  pamoja na watunga sera.

0/Post a Comment/Comments