JESHI LA POLISI VIWANJA VYA NDEGE LA KAMATA HEROIN NA VIDANI VILIVYOTENGENEZWA NA MENO YA TEMBO VYENYE TAMANI YA TEMBO MZIMA

Kamanda wa Polisi  wa  Viwanja  vya  Ndege  Tanzania  Jeremia  Shila wakati  akitoa  taarifa  ya  kukamatwa  kwa  Raia   mmoja  wa  China  aliyekutwa  na vidani  na bangili vilivyotengenezwa  kwa meno ya tembo vikiwa  na  tahamani  ya  Tembo  mzima

............................

NA SALYM BITCHUKA

Jeshi  la  polisi  Viwanja  vya  Ndege  Tanzania  limesema litahakikisha  linawatia  nguvuni  na kuwafikisha  katika  vyombo  vya  sheria  wale  wote   wanaojihusisha  na  kusafirisha  madawa  ya  kulenya  na  nyara  za  Serikali  katika  uwanja  wa  ndege  wowote  hapa  nchini.

Kauli  hiyo  imetolewa  leo  jijini  Dar  es Salaam na  Kamanda wa Polisi  wa  Viwanja  vya  Ndege  Tanzania  Jeremia  Shila wakati  akitoa  taarifa  ya  kukamatwa  kwa  Raia   mmoja  wa  China  aliyekutwa  na vidani  na bangili vilivyotengenezwa  kwa meno ya tembo vikiwa  na  tahamani  ya  Tembo  mzima .

Kamanda  Shila  amesema  mtuhumiwa  huyo  Raia   wa  China amefahamika  kwa  jina la   Dong  Weijuan (44)  alikuwa  akisafiri  kwenda  Bang kok  Thailand  ambapo  alikamatwa  katika  uwanja  wa  Ndege  wa  Kimataifa  wa Julias  Nyerere ( JNIA).

‘Raia huyo mwenye umri wa 44 aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya Qatar mruko namba QR 1499 majira ya saa 10:00kwenda BANGKOK,THAILAND akiwa na vidani kumi na bangili moja vilivyotengenezwa kwa meno ya Tembo vyenye uzito wa gramu 110,pia alikutwa na bangili nyingine moja iliyotengenezwa na manyoya ya mkia wa Tembo (Singa) vyote vikiwa na thamani ya tembo mzima’amesema Kamanda Shila

Katika  tukio  lingine  Kamanda  Shila  amesema  jeshi  la  Polisi Viwanja   vya ndege  limefanikiwa  kumkata  Raia   mmoja  wa  India aliyefahamika  kwa  jina    Paokholen  Lhungdim ( 23) akiwa  na  madawa  ya  kulevya  aina  ya  HEROIN  yenye  uzito  wa   Kg 17 .40.

Sanjari  na  hayo  Shila  amesema  katika  msimu  huu  wa  Sikukuu  za Eid El Fitri  jeshi  hilo  limejipanga  vizuri  katika  kuimarisha ulinzi  maeneo  yote  ya  Viwanja  vya  ndege  huku  akiwaomba  wananchi   waishio  karibu  na  Viwanja  vya  ndege  kutoa  ushirikiano  kwa  Jeshi la Polisi  katika  jukumu la   ulinzi

0/Post a Comment/Comments