KAMPUNI YA MCHONGOO YAJA NA MIKAKATI YA KUWAINUA VIJANA KUPITIA WEBSITE YA MCHONGOO


Mkurugenzi  Kampuni  ya mchongo, Julias Wambogo (kulia) akiwa na Fayaz Diamond Valli Mkurugenzi wa Tech Advisor na Mshauri ufundi wa Kampuni ya Mchongoo (kushoto) wakizungumza na waandish wa habari kuhusu uzinduzi  wa    Website  ya  Mchongoo.

........................

NA SALYM BITCHUKA 

Katika  kuhakikisha  vijana  wa  Kitanzania wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na tatizo la ukosefu wa Ajira, Kampuni  ya  mchongoo ltd  imeanzisha  jukwaa la  kuwasaidia  watanzania  wenye  ujuzi. 

Haya  yamebainishwa  Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi  Kampuni  ya mchongo, Julias Wambogo wakati akizungumza na waandish wa habari kuhusu uzinduzi  wa    Website  ya  Mchongoo  ambao itakuwa na jukumu la watu mbalimbali wenye ujuzi kujitangaza.

Wambogo amesema sababu iliyomtuma kuanzisha Website  hiyo  ni baada ya kuona vijana wengi wa kitanzania wakihangaika kwa kukosa fursa huku wakiwa na ujuzi mbalimbali.

'' watu  wote wenye ujuzi wa  fani mbalimbali wanaruhusisiwa kuainsha kazi zao  wanazofanya na website hii itawawezesha kuonekene  kwa  urahisi  zaidi" amesema  Julias Wabongo. 

Aidha,Wambogo amewataka vijana kuchangamkia fursa hyo kwa kwa jiunga na Mchongoo Website  pamoja makampuni mbalimbali kujitokeza kutumia jukwaa hilo  ili  kujipatia wataalamu mbalimbali.

0/Post a Comment/Comments