KCB BANK YAZINDUA HUDUMA ZA BIMA NCHINI

 


Na Mwandishi wetu

Wafanyakazi na wadau wote wa bima nchini wameombwa kuunga mkono  jitihada  zinazoendelea kufanywa na banki ya Kcb katika kuongeza uelewa na upatikanaji rahisi  wa bima kwa watanzania wote

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam  wakati  wa hafla ya uzinduzi wa bima kwa Bank ya KCB, mkuu wa idara ya wateja wa rejareja ,wadogo na wakati, wa bank hiyo Abdul Juma amesema kuwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania na Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) wamepewa rasm  mamlaka ya kutoa huduma za bima kutoka bank kwenda kwa mteja hivyo kuanzia sasa watu wote wanaweza pata huduma hiyo hata kwa mkopo wa kulipa kidogo kidogo.


Aidha Huduma za Bima za KCB zitakuwa katika makundi tofauti kama vile bima ya maisha pamoja, bima za magari, za vikundi na nyinginezo.


Kwa upande wake mkuu idara ya masoko na mawasiliano ,KCB BANK Christine Manyenye amesema kuwa  uzinduzi wa huduma hiyo ni mwendelezo wa ubunifu na kuangalia mahitaji ya wateja wao.


Utambulisho wa Huduma za Bima za KCB unakuwa ni muendelezo wa huduma nzuri na zenye viwango kutoka KCB bank.

0/Post a Comment/Comments