MAKAMPUNI BINAFSI YA ULINZI YENYE MAPUNGUFU YAONYWA

 



Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzania limesema halitasita kuyachukulia hatua kali za Kisheria Makampuni yote ya ulinzi Binafsi yenye mapungufu ya kisheria.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara malum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni operation endelevu la kukagua ukaguzi katika makampuni hayo.

 Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzani ACP Issack Katamiti amesema kuwa kama watabaini kuwa kuna makampuni hayafuati sheria, taratibu na kanuni na miongozo inayotakiwa ambayo miongozo inatolewa na mamlaka za serikali.


Kwa upande wa Meneja msaidizi Mamlaka ya Mapato ( TRA) Dodoma Silver Rutagwelera  amezitaka kampuni zote binafsi za ulinzi kutunza kumbukumbu zao zote kitendo kinachopelekea kutambulika kwa urahisi utendaji kazi wao.


"Tunaangalia makadirio na mapato, uwasilishaji wa  return za mwezi au mwaka,mikataba ya malindo na jengo,paylow, mishahara ya wafanyakazi ili kuweza kubaini kama kodi inayokatwa na kuwasilishwa kwetu pamoja na mengine yanayoweza jitokeza" alisema Rutagwelera




Naye Alice Milanzi kutoka Idara ya Kazi mkoa wa Kazi Temeke  amesema kuwa wamekuwa wakiangalia mambo mbalimbali ikiwemo stahiki zao mbalimbali kwa kujibu wa sheria ikiwemo ikiwemo mikataba ya kazi, paylow ili kujiridhisha kama wafanyakazi wanalipwa sawa kulingana na kazi wanayofanya.


 Katika hatua nyingine  msimamizi wa uandikaji kutoka mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), Hassan Dotto amesema kuwa wamekuwa wakifuatilia mishahara inayolipwa kama inaendana na kinachowasilishwa katika mfuko huo.


Imeelezwa kuwa waajiri wote na waajiriwa wa kampuni za ulinzi wametakitakiwa kuhakikisha kuwa wameungwa katika mfumo wa PSGB


.






0/Post a Comment/Comments