MKURUGENZI MKUU WA MAKUMBUSHO YA TAIFA DKT LWOGA AWATAKA WASANII KUCHANGAMKIA MAJUKWAA KUTANGAZA KAZI ZA SANAA.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa DKT Lwoga akizungumza na waandishi wa habari.
Dkt Noel  Lwoga akipokea picha kutoka kwa Mwamtumu Mburku Mwanafunzi wa TASUBA
Naibu Mkurugenzi Mkuu Tanzania bora Initiative ambayo ni sehemu ya Sanaa pamoja program kwa kushirikiana na Nafasi Arts Space Bw.Isma
.................…...

Na Richard Mrusha

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amewashauri Wasaniii kupenda kutumia majukwaa au midahalo mbalimbali kuonyesha kazi zao ili kuwasaidia kujitangaza na kutimiza ndoto zao.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya "Sanaa kwa Pamoja inayotekelezwa na Nafasi arts Space kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kutanua wigo wa kazi zao na kuleta uwiano wa pamoja kwa vijana katika kazi za Sanaa.

Dkt Lwoga amesema kwamba majukwaa yanayowakutanisha wasanii wa ndani na nje ya Nchi yanasaidia wasanii kutangaza vipaji vyao na kuviendeleza hivyo kuwafanya kujitengenezea ajira na kujipatia kipato Ili kuweza kwa lengo la kujikumu kuwapunguzia utegemezi kwa wazazi walezi wao", amesema

"Iko haja sasa wasanii hawa wakatengenezewa majukwaa endelevu kwani walio wengi wanategemea kupitia majukwaa hayo kwa lengo la kuonyesha kazi zao na zikionekana wanajipatia kipato kupitia watu watakaovutiwa na kuweza kuzinunua "amesema Dkt Lwoga

Nakuongeza kuwa "taratibu taratibu kadri siku zinavyozidi kuendelea wasanii wa Tanzania wanaendelea kuvuka mipaka kimataifa na kuipeperusha bendera ya nchi kupitia majukwaa na midahalo mbalimbali ,hivyo Serikali imekua bega kwa bega kuhakikisha vipaji chipukizi vinatengenezewa mazingira wezeshi. 

Na Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu Tanzania bora Initiative ambayo ni sehemu ya Sanaa pamoja program kwa kushirikiana na Nafasi Arts Space Bw.Ismail Biro amesema kuwa kupitia programu hiyo iliyozinduliwa itasaidia kuwasogeza wasanii pamoja kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ikiwemo wanaoshiriki Sanaa Kwa vitendo,nadharia ili kusaidia kazi zao kuwa bora kimataifa

"Tutawatengenezea mazingira rafiki wasanii ya kuweza kupata fursa kupitia kazi zao wanazozifanya kwa kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa Maendeleo ndani na nje ya nchi ili waweze kuwasaidia pale wanapokuwa na changamoto yoyote ili wafikie malengo wanayokusudia "amesema Bw.Ismaili

Kupitia Uzinduzi wa Programu ya "Sanaa Kwa pamoja"baadhi ya kazi za Sanaa ya uchoraji zimepokelewa na kuhifadhiwa kwenye Makumbusho ya Taifa ambapo miongoni mwa msanii aliyekabidhi kazi hizo ni Mwanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) Mwamtumu Mbaruku ambapo amewaasa vijana kujitokeza kuonyesha vipaji vyao.

"Na Kwa upande wake mwanafunzi aliyeonyesha picha yake anasema ninajisikia furaha sana picha yangu niliyoichora kupokelewa na kuhifadhiwa hapa makumbusho ya Taifa Mimi ni mwanafunzi mdogo na ni msanii mchanga nataumaini kupitia majukwaa ya Sanaa nitafika mbali na kutimiza ndoto yangu. amesisitiza Mwamtum

Naye Balozi wa Uswis Nchini Tanzania Didier Chassot amesema Ubolozi huo umetenga kiasi cha fedha ambacho kitakuwa chachu ya kuweza kuwasaidia wasanii ikiwemo wasanii wa nyimbo,Sanaa za maonyesho,Sanaa za uchoraji nazinginezo hivyo wasanii hao wachangamkie fursa hiyo.

Aidha Programu hiyo ya Sanaa Kwa Pamoja imefadhiliwa na wadau mbalimbali wa Maendeleo ikiwemo Umoja wa Ulaya(EU),Ubalozi Norwey ,pamoja na Ubalozi wa Uswis, huku ikiwa na lengo la kusaidia kuzungumzia changamoto katika sekta ya sanaa na jinsi ya kuzitatua ili kuikuza sekta hiyo na kutengeza ajira kwa vijana.

0/Post a Comment/Comments