Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, limewakumbusha viongozi wa nyumba za ibada na sehemu za starehe kuzingatia sheria za viwango vya kelele.
Agizo hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mkuu wa NEMC Dkt Samweli Gwamaka, wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kusema kuwa sehemu yoyote itakayokiuka itafungiwa mara moja kwa kukiuka sheria hiyo.
Amesisitiza kuwa hivi karibuni wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu mbalimbali, juu ya ukiukaji wa sheria ya kiwango cha kelele kutoka kwenye bar na nyumba za ibada hali ambayo inaleta kero kwa wananchi.
Gwamaka amesema, wamekuwa wakitoa viwango vya upigaji wa kelele kwa muda wa usiku na mchana, hivyo kwa atakayekiuka agizo hilo watawafungia au kuwachukulia vifaa vyao na kuwapeleka Mahakamani kwa kosa la kuvunja sheria ya viwango vya kelele.

Post a Comment