*********************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* na balozi wa Mazingira kupita Kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es salaam *Msanii Ally Selehe Kiba* almaarufu Kama *Alikiba* wamefanya *Usafi wa pamoja* eneo la Tabata ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Mkoa kufanya Usafi *kila Jumamos ya mwisho wa Mwezi.*
Akizungumza wakati wa zoezi Hilo lililokwenda sambamba na bonanza, *RC Makalla* amepongeza Wakazi wa Dar es salaam kwa *mwamko mkubwa wa kufanya Usafi* jambo linalofanya Jiji Hilo kushika *nafasi ya sita kwa Usafi Barani Africa*.
Aidha *RC Makalla* amempongeza *Msanii Alikiba* kwa kuratibu vizuri zoezi la Usafi wa pamoja siku ya Leo kwa kushirikiana na *vikundi mbalimbali.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* ametumia hafla hiyo kuwahimiza Wananchi *kuheshimu Mambo matano* yaliyokatazwa ikiwemo Ufanyaji biashara kwenye *maeneo yaliyokatazwa*, biashara kwenye *njia ya watembea kwa miguu, hifadhi ya Barabara,* Ufanyaji biashara *juu ya Mitaro* pamoja na Ufanyaji biashara *mbele ya Taasisi za umma* ikiwemo Shule.
Hata hivyo *RC Makalla* amepokea *msaada wa Vifaa mbalimbali vya Usafi* kutoka kwa *Wadau* walioguswa na jitiada za Mkoa katika *kusafisha mazingira* kupitia Kampeni ya *Safisha Pendezesha Dar es salaam.*
Kwa upande wake *Msanii Alikiba* ameahidi kuendelea kushirikiana na *RC Makalla* katika kuhakikisha *Jiji la Dar es salaam linaendelea kuwa safi* ambapo ametoa wito kwa *Wananchi kufanya Usafi*.


Post a Comment