Serikali imetangaza msamaha wa riba kwa waajiri wote waliochelewesha kuwasilisha michango katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC).
Akitoa tamko hilo leo jijini Dar es salaam, waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu, kazi, vijana, ajira na wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 75(5) cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi (sura 263) anatangaza msamaha wa riba iliyoanza kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01, Oktoba,2017 hadi 31 Agosti 2021 kwa waajiri wote waliochelewa kuwasilisha michango katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwa kipindi hicho.
Aidha amesema kuwa watakaonufaika na msamaha huo ni wale waliokwisha lipa malimbikizo ya michango wanayodaiwa na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi na wamebakiza deni la riba pekee yake.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Dkt. John Mduma ameishukuru serikali kwa kukubali kutoa punguzo hilo kwani litarahisisha usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo.
Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF), ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa kujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi, sura 263 kwa lengo la kushughulikia masuala ya Fidia kwa wafanyakazi walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania bara ambao wataumia,kuugua am kufariki kutokana na kazi.


Post a Comment