TCAA YAIUNGA MKONO SHULE YA ALPHA KWA KUANZISHA MAFUNZO YA USALAMA WA ANGA.

 


        *****************************

Na Richard Mrusha

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na mama Tunu Pinda ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa  awamu ya nne Mizengo Pinda ,wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa programu maalumu za mafunzo ya anga zilizoanzishwa na Shule ya  Alpha.


Amesema kwasasa hakuna Mitaala rasmi ya kufundisha masomo yanayohusu Sekta ya anga akitolea mfano masuala ya uhudumu wa ndege,uhandisi au urubani ambapo vijana wengi  wamekua wakipoteza ndoto zao hivyo serikali haina budi kuanzisha Mitaala hiyo ili vijana wengi wasome masomo hayo wakiwa bado wadogo.



"Shule ya Alpha imefanya jambo la msingi sana kuanzisha program hizi ambazo zitasaidia vijana wanaopenda kusomea mambo ya anga mfano urubani,uhudumu wa ndege ili watimize ndoto zao,naomba kutumia fursa hii kuiomba serikali ianzishe Mitaala rasmi ya masomo ya anga  kuanzia shule za Sekondari ili kusaidia vijana kutimiza ndoto zao" amesema mama Tunu Pinda


Hata hivyo Bi.Maria ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya anga nchini(TCAA) amesema kwamba mamlaka hiyo imefurahishwa na uthubutu wa shule ya Alpha kuanzisha mafunzo ya usalama wa anga kwani itasaidia kuzalisha watalaamu wengi wa anga.


"Kuanzisha mafunzo kwa levo ya sekondari itasaidia wazazi kumudu gharama za kusomesha,lakini pia tutakuza soko la wataalamu wa mamlaka ya anga ,kwetu sisi kama TCAA tunaona hawa ni waajiriwa wa soko letu la usafiri wa anga ,tunaipongeza sana shule ya Alpha na tupo tayari kufanya nao kazi kwa pamoja kwani tunachuo chetu ambacho kinazalisha wataalam mbalimbali" amesema Bi Maria ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TCAA.


Nakuongeza kwamba " Sisi Mamlaka ya anga(TCAA)tumeanza mazungumzo na Shule ya Alpha kuona ni namna gani tunaweza kiunganisha nguvu ili tuweze kuzalisha wataalamu wengi kwani kwa sasa bado tuna uhaba mkubwa wa wataalamu wa usalama wa anga. 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule ya Alpha Bi.Fatina Senzota amesema kwamba shule hiyo imeamua kuanzisha program za mafunzo ya sekta ya anga ili kuwasaidia vijana kuanza kujifunza wakiwa na umri mdogo hatua hiyo itasaidia kufanikisha ndoto ya vijana wengi wanaopenda kufanya kazi katika sekta ya anga.


"Tunashirikiana na Kenya School of airline, pamoja na Shirika la ndege la uturuki (Turkish airline)kutoa mafunzo haya kwa vitendo tunamini vijana wengi wanaopenda kuwa marubani ,wahandisi katika masuala ya anga au wahudumu wa ndege,sasa inapendeza wajifunze wakiwa wadogo kuanzia  shule ya sekondari,kidato cha nne hadi sita." amesema Mkurugenzi huyo.


Nakupongeza  kwamba "Wanafunzi kutoka shule zingine watakaopenda kujifunza  programu za mafunzo ya  anga tutaweka utaratibu waweze kuja kusoma hata kama ni vipindi vya jioni lengo letu ni kusaidia vijana wengi wanaotamani kuwa wataalamu wa masuala ya anga watimize ndoto zao.


Nae Joel Lulandala mwanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo ambaye anasoma programu za mafunzo ya anga shuleni hapo amesema kwamba kozi hizo zinawasaidia vijana kutambua  vipaji vyao( Carrier) nakwambia kuwafanya waweze kufanikisha malengo yao.


" Mimi binafsi nilipenda sana kuwa rubani ,ndo maana nasoma program hizi hivyo nawaonba vijana wanaopenda kusoma kozi hizi waje wajifunze" amesema mwanafunzi huyo kwa furaha.

0/Post a Comment/Comments