DAR KINARA MIGOGORO YA ARDHI

 


         
WAZIRI Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula


               *****************************


WAZIRI Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umekithiri kwa uvamizi wa ardhi hasa kwa baadhi ya wananchi kununua maeneo na kuyaendeleza bila kujua uhalali wa umiliki wa eneo husika.

Waziri Mabula ameyasema hayo  jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano ulioikutanisha Wizara hiyo na jukwaa la  wahariri wa vyombo vya habari (TEF.)

“Hali ya uvamizi wa ardhi kwa Mkoa wa Dar es Salaam imekithiri kwa kiasi kikubwa, watu wana hati za umiliki wa maeneo lakini hawataki kuendeleza maeneo hayo…Wanatokea wajanja wanauza eneo hilo kwa mtu mwingine ambaye haulizi uhalali wa eneo hilo kwa ofisi husika anajenga kumbe amevamia eneo la mtu….” Amesema.



Aidha amesema kuwa, ni vyema wananchi wakazitumia ofisini za ardhi zilizopo kote nchini wakitaka kujenga au kuendeleza maeneo kabla ya kukumbana na kadhia ya uvamizi pindi sheria inapofuata mkondo wake.

0/Post a Comment/Comments