G7 KUISAIDIA UKRAINE DHIDI YA URUSI


""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Viongozi wa nchi za kundi la G7 wameapa kufanya gharama ya vita kuwa ghali zaidi kwa Urusi ili kuiunga mkono Ukraine. 


Katika taarifa yake ya kuufunga mkutano wa kilele wa G7 uliofanyika katika mji wa Elmau katika jimbo la Bavaria, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema Rais Vladmir Putin wa Urusi lazima asishinde vita hivyo. 

Hatua muhimu iliyofikiwa katika mkutano huo ni kuweka ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi ili kupunguza mapato ya nchi hiyo. 


Licha ya vikwazo kutoka kwa nchi za Magharibi, mapato ya mafuta ya Urusi yaliongezeka mwezi Mei. 

India na China pia zimeongeza pakubwa manunuzi yao ya mafuta ghafi ya Urusi tangu vita vilipoanza. 


Mataifa ya G7 pia yaliahidi dola bilioni 4.5 za kusaidia upatikanaji wa chakula duniani.

 Vita nchini Ukraine vimezuia usafirishwaji wa ngano, mafuta ya alizeti na mahindi hasa kwenda Afrika. 

Mashirika ya misaada yanaonya kuwa baadhi ya maeneo ya Afrika huenda yakakumbwa na njaa hivi karibuni huku vyakula vikipungua.


#Dwkiswahili

0/Post a Comment/Comments