DKT NUNGU : BUNIFU NA TAFITI KUENDELEA KUWEKEWA MAZINGIRA WEZESHI NCHINI


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akizungumza katika fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika Juni 25,2022 Chuoni hapo.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akikabidhi vyeti na zawadi kwa washindi wa fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika Juni 25,2022 Chuoni hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye pamoja na baadhi ya viongozi wa Chuo hicho wakiwa Kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Fainali za shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika Juni 25,2022 Chuoni hapo.
 
...................

Dar es Salaam. 

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk Amos Nungu amesema, Serikali kupitia Tume hiyo, imeweka mazingira mazuri ya Ubunifu na Tafiti ili kuhakikisha wabunifu wanafikia malengo waliokusudia. 

Dkt. Nungu amesema hayo  25 Juni 2022 kwenye fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiriamali la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UD AIEC 2022) lililofanyika katika ukumbi wa Nkrumah. 

Kutokana na hilo Dkt. Nungu amewafunda washiriki pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu huku akiwataka kutokata tamaa hususani wanapokumbana na changamoto mbalimbali.

Ukiacha hayo Mkurugenzi Mkuu amekabidhi zawadi kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza ni Timu ya Upcyclers ambao wamepata sh milioni 10 huku wa pili ni timu ya UBVC21 waliopata sh milion 7.5 wakati mshindi wa tatu ni timu ya Agrozaidi waliopata sh milioni 5.

Dkt Nungu amesema washindi hao pia watapata nafasi ya kujiunga na kituo cha uatamizi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilicho chini ya Kurugenzi ya Ujasiriamali na Ubunifu.

0/Post a Comment/Comments