Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Amos Makalla akizungumza na
waandishi wa habari leo Juni 29,2022 katika Ofisi za Habari Maelezo JNICC
Jijini Dar es Salaam. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu
........................................
NA MUSSA KHALID
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani
yatakayofanyika Julai 7 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa maadhimisho hayo ambayo yatafanyika kwa mara ya
kwanza Dunia, Julai 06 yatatanguliwa na kongamano la mchango wa lugha ya
Kiswahili katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika likihusisha Viongozi
kutoka ndani na nje ya Nchi.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Amosi Makala wakati akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa kushirikiana na
Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kuandaa tamasha la utamaduni la kwanza
kitaifa pamoja na siku ya Kiswahili Duniani.
Aidha RC Makalla amesema Julai 04 Kutakuwa na maandamano ya Amani
kuhusu Lugha ya Kiswahili na Utoaji haki kutoka Temeke mwisho mpaka Uwanja wa
Uhuru ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Damas
Ndumbaro.
Awali Mkuu Mkoa Makala amesema kuanzia Julai 1-3 mwaka huu Wizara
ya utamaduni,Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa
tamasha la utamaduni la kwanza kitaifa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
‘Julai 03 kutakuwa na Usiku wa Taarabu katika ufukwe wa Coco Beach
ukihusisha burudani ya Mziki mwanana kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo
Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Patricia Hilary, Mzee Yusuph na wasanii na vikundi
ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson’amesema RC
MAKALA
RC Makala amesema kuwa kuandaliwa kwa tamasha hilo ni utekelezaji
wa maagizo ya Rais Samia Suluh Hassn aliyoyatoa mkoani Mwanza Septemba
8,2021 katika tamasha la utamaduni ambapo aliagiza ‘Matamasha hayo yafanyike
kwa mzunguko kila mkoa ili watanzania waweze kujua mila na desturi za kila mkoa
na kila pembe ya Tanzania.
Tamasha hilo litakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Utamaduni wetu,Fahari yetu,tujiandae kuhesabiwa kazi iendelee’hivyo watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutambua,kuthamini,na kuendeleza urithi wao


Post a Comment