RC MAKALLA: BANK YA AFRICA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA MASOKO YA KISASA YA MACHINGA


.....................

- Ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za *Rais Samia kuboresha mazingira ya Machinga.*

- Awaelekeza *Wakuu wa Wilaya/ Wakurugenzi kuweka Mkazo jambo Hilo.*

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amefanya kikao baina ya *Bank ya Maendeleo ya Africa* ADB na Viongozi wa Mkoa wa *Dar es salaam, Dodoma, Wizara ya Fedha, TAMISEMI na TANROAD* kujadili ofa iliyotolewa na Bank hiyo ya *Ujenzi wa Masoko ya kisasa* kwaajili ya Machinga kwenye *Wilaya zote tano za Mkoa huo.*

Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, *RC Makalla* amesema Bank hiyo imeamua *kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita* kuboresha mazingira ya *Machinga walioamua kuitikia wito wa Serikali kufanya biashara kwenye maeneo waliyopangwa.*

Ili kufanikisha Mpango huo unaokwenda *kuchochea* biashara, *RC Makalla* amewaelekeza *Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi* kumkabidhi taarifa kamili inayoainisha *Wapi Masoko hayo yajengwe, Michoro na Gharama* halisi kabla ya ijumaa ili awasilishe kwa Bank hiyo kwaajili ya *utekelezaji.*

Pamoja na hayo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD, TARURA, DAWASA, TANESCO, LATRA* kuhakikisha kuanza maandalizi ya kuhakikisha Maeneo yanapojengwa Masoko hayo yanakuwa na *huduma zote muhimu* ili kuchochea biashara.

Kwa upande wake *Meneja* Wa Bank ya maendeleo Afrika tawi la Tanzania *Patricia Laverley* amesema kuwa *Bank hiyo ipo tayari* kutekeleza Ujenzi wa Masoko hayo kwakuwa wameguswa na jitiada za *Rais Samia Suluhu Hassan* katika kuhakikisha Wafanyabiashara wanaendesha biashara kwenye *maeneo sahihi na Bora.*

0/Post a Comment/Comments