TMA YATAHADHARISHA ATHARI KATIKA KIPINDI CHA KIPUPWE

 


Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dkt Ladislaus Changa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dara es salaam.

          

       ***************************

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA,  imesema  katika kipindi cha mwezi June,Julai na Agost 22 hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi.

Akitoa taarifa ya mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni –Agost (JJA)2022, Mbele ya waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es salaam, kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dkt Ladislaus Changa amesema  kuwa hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini pamoja na nyanda za juu kaskazini mashariki.

Amesema kuwa vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza mwezi Juni na julai huku vipindi vya baridi kali vikitarajiwa katika maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kusini magharibi hususani nyakati za usiku na asubuhi.

Aidha amesema athari za magonjwa ya mifugo yanayoambatana na baridi kama vile homa ya mapafu yanaweza kujitokeza na hali ya vumbi inayoambatana na upepo mkali katika baadhi ya maeneo inatarajiwa kujitokeza na kuathiri afya ya binadamu na wanyama.

Hata hivyo wananchi wameshauri kuendelea kufuatilia mara kwa mara taarif aza hali ya hewa.

0/Post a Comment/Comments