TMDA YAKAMATA DAWA ZISIZO NA USAJILI ZA MAMILIONI DAR

 


**************************************



Dar es Salaam.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekamata dawa ambazo hazijasajiliwa zenye thamani ya TSh 294,486,590 milioni ambapo tozo yake inakaribia kuwa 80 Milioni.

Zimekamatwa kufuatia ukaguzi maalum,   uliofanyika eneo la Mtaa wa Kitumbini katika Kata ya Mchafukoge katikakati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika eneo la tukio, Meneja wa Kanda wa TMDA, Bw. Adonis Bitegeko alisema,

"Timu ya TMDA Kanda ya Mashariki, tumekamata ghala bubu ambalo halijasajiliwa na TMDA,

Tumebaini ghala hili ambalo lipo chini ya mmiliki wake Bw. Amaiya Rijendra likiwa limehifadhi dawa mbalimbali za binadamu ambazo hazijasajiliwa.

Tulichokifanya wenzetu jeshi la Polisi wanemchukua mtuhumiwa kwaajili ya hatua zaidi na TMDA tumekusanya dawa zote ambazo hazijasajiliwa na kuzichukua".

Ambapo ameongeza kuwa, wamechukua taratibu za kuziorodhesha na hatua kadhaa za kisheria ikiwemo kuwatoza faini na pia watatakiwa kulipia gharama za kuziteketeza",

Aidha, TMDA tunatoa onyo kwa wanaoendelea kufanya biashara hiyo haramu kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo pia amewaonya pia wataalamu husika wanaojihusisha na biashara hizo haramu kuwa hawatosita kuwafutia leseni zao  za kitaaluma

Meneja wa Kanda amezitaja baadhi ya dawa zilizokamatwa kuwa ni pamoja na

Dawa za magonjwa ya shinikizo la damu, dawa za kutoa ujauzito na  dawa nyingine tofautitofauti." Alisema.

"Rai yetu ni kwamba wale wote wanaofanya biashara haramu adhabu ni kali na hawatamuacha mtu", alimalizia

Zoezi hilo lilikuwa la usiku kucha, na kumalizika Asubuhi ya tarehe Juni 28, 2022

Mtuhumiwa aliyekutwa nazo ni mtanzania mwenye asili ya India ambapo alipohojiwa alikiri kuendesha ghala hilo bubu pasipo na kibari na kinyume na sheria kwa kile alichodai hakufahamu mamlaka husika za usajili, 

Dawa hizo ziliweza kuchukuliwa na TMDA kwenye magari Kwa ajili ya hatua zaidi.





Mwisho.

0/Post a Comment/Comments