Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akitazama moja ya kifaa malumu cha kujifunzia utengenezaji wa ndege kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akikata utepe kuzindua chumba maalumu cha kufanyia majaribio kwa vitendo kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam
********************************
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezundua vifaa vitatu vya uhandisi wa matengenezo ya ndege vinavyo ghalimu zaidi ya Sh. Bilioni 2 katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kuzalisha wataalamu wenye weledi mkubwa.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vifaa hivyo katika chuo cha taifa Cha Usafirishaji (NIT), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, amesema kupitia mradi wa kukuza ujuzi ambao upo kwenye nchi tatu za Afika Mashariki wameweza kupata fedha kutoka benki ya dunia na kununua vifaa hivyo.
Amesema vifaa hivyo vitatumika vizuri kuwapa ujuzi wenye weledi mainjinia wanaohusika kutengeneza ndege, ambapo wataweza kufanya kazi za mikono, kwa sababu anapofundishwa lazima ashike chombo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Zacharia Mganilwa amevitaja vifaa hivyo kuwa ni kompyuta za kisasa ambazo zinatumika kufundishia wahandisi wa ndege duniani.


Post a Comment