WADAU WAENDELEA KUPAZA SAUTI KUHUSU MTOTO KULINDWA NA KUPEWA HAKI ZAKE.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga wilaya humo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya mwanamke na mtoto akizungumza na wanahabari akiwaeleza umuhimu wa Siku ya Mtoto wa Afrika.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Women Journalist Advocates For Children Right (TAWOJAC ) akizungumza na wanahabati katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.

Inspekta Blandina Ndunguru kutokea Dawati la Jinsia na watoto Changombe akizungumzia siku ya Mtoto wa  Afrika

Baadhi ya wanafunzi na wadu mbalimbali ambao wamejitokeza kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.(picha na Mussa Khalid)

...........................

NA MUSSA KHALID

Jamii nchini imetakiwa kuwa na maadili ya kuimarisha ulinzi wa watoto kwa kutokomeza ukatili dhidi yao ili kuweza kutengeneza taifa bora la kesho.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya Jokate amesema kuwa ili kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na haki zao serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuunda mabaraza ya watoto kwenye mitaa na kata zao ili kutoa nafasi kwa watoto kujadili mambo yanayowahusu na changamoto zinazowakabili.

Aidha amewataka wazazi  na walezi kuhakikisha  wanaimarisha ulinzi kwa watoto pamoja na kuwapatia haki zao za msingi hatua itakayochangia malezi bora pamoja na kuimarisha makuzi ya akili .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya mwanamke na mtoto ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema umuhimu wa siku hiyo wanakwenda kuweka nguvu kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa katika jamii mbalimbali.

Amesema katika kuhusiana na masuala ya ukatili wa watoto katika Halmashauri ya Temeke wamekuwa wakionyesha juhudi ya kuyatokomeza licha ya kutokea baadhi ya matukio lakini wameyadhibiti.

Naye Inspekta Blandina Ndunguru kutokea Dawati la Jinsia na watoto Changombe amesema ukatili wa watoto umekuwa ukijitokeza katika kutoka na jamii kutokuwa na elimu hivyo wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu ili kupambana na ukatili huo.

Magreti Kyando ni Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOJAC amesema kwa mujibu wa takwimu ambazo zilitolewa zinaonyesha ukatili umekuwa ukiendelea huku baadhi ya wanafunzi wakiiomba serikali kuvidhibiti vitendo hivyo vya kikatili.

Kwenye Maadhimisho hayo wameshiriki wadau mbalimbali wakiwemo Watetezi WA Haki za Binadamu ambapo Kauli mbiu ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa Kila June 16 mwaka huu yanakwenda sambamba na kauli mbiu ya kitaifa isemayo ‘Tuimarishe Ulinzi wa Mtoto,Tokomeza ukatili dhidi yake,jiandae kuhesabiwa’q

0/Post a Comment/Comments