Na. Dominic Haule,
Askofu Msadizi wa Jimbo kuu katoliki la Dar es salaam Mhashamu Stephano Msomba, Amewata wakristo kuendelea kutanga Ufalme wa Mungu kwa Viumbe wote waliopo hapa Ulimwenguni ili waweze amini na kumfata kristo.
Askofu Msomba wito huo Ameutoa hivi karibuni Kupitia Homilia ya Misa Takatifu kwa Waaminia Waamini wa Parokia ya Mt. Veronica Mwanagati Jimbo kuu la Dar es salaam, ambapo pia amewapatia Sakramenti ya Kipaimara Vijana 44 Parokiani hapo.
Askofu Msomba alisema kuwa Kila mkristo mbatizwa anapaswa kutangaza neno la Mungu Badala ya kujikita kutanga mambo mengine ambayo hayaendani na Ujumbe Mungu.
Wakati huo huo Amewasihi wakristo kuwaita majina mema Watoto wao ambayo yenye kumtukuza Mungu Badala ya kuwaita majina ambayo hupelekea huchochea kutenda maouvu katika maisha yao siku zote wawepo hapa Ulimwenguni.
Hatahivyo Askofu Msomba alisema kuwa Kila mkristo ajiulize namna gan anashiki kuihubili Habari njema ya Kristo pamoja na kueneza Ujumbe wa Mungu katika maisha yake ya Ukristo hapa Duniani.
Aidha Askofu Msomba Amewata wakristo kuwa watu wa kutii Neno Mungu linavyo eleza kwakufanya hivyo litamsadia mkristo kukua kiroho na kuwa mkristo hodari wakumtangaza Kristo.
Pia ali sema kuwa wazazi na walezi wamehimizwa kuendelea kusoma Neno la Mungu na Watoto wao ili waweze kuwa Imara katika Imani na kuto yumbishwa na watu Wengine wanao kutana nao hapa Ulimwenguni.
Katika hatua nyingine Amewasihi Vijana waliopata Sakrament ya Kipaimara kuendelea kuwa askari hodari wa kumtangaz kristo pale popote wawapo hapa Duniani kwakuwa Wana Roho wa Mungu katika Maisha yao.
Askofu amehitimisha Homilia yake kwa na kuwataka Vijana hao 44 hao waliimalishwa leo kuendelea kusoma Maandiko matakatifu Kila wakati ili waweze kukua kiroho na kuwafundisha Wadogo zao na hatimayae wawe askari hodari wakristo.
Misa hiyo iliongozwa na Askofu Msadizi Jimbo kuu katoliki la Dar es salaam Mhashamu Stephano Msomba akishikiana na Padre John Mallya Kaimu Paroko wa Parokia ya Mt. Veronika Mwanagati iliyopo Dekania ya Ukonga Jimboni humo.







Post a Comment