WANAOJIUZA WHATSAPP NA FACEBOOK WAKAMATWA DAR

 



**********************************

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam imewakamata watu wawili kwa tuhumiwa za usambazaji wa picha za ngono na kuuza mwili kwa njia ya Mtandao ya kijamii ikiwemo facebook, WhatsApp, Tinder na Exotic tz.

Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam Murilo Jumanne amesema watuhimiwa hao ni Marry Samson Sibora maarufu Asha Zungu ( 23), Mzanaki, mkazi wa Sinza Mugabe na Zainabu Yahaya Omary maarufu official Manka ( 23), Mrangi, mkazi wa Buguruni.


Kamanda Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na Timu maalum ya kuzuia na kupambana na uhalifu mtandaoni, imefanya Oparesheni maalum kuanzia May 18,2022 hadi June 26,2022 na wamehojiwa kwa kina na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe Mahakani haraka iwezekanavyo.

0/Post a Comment/Comments